Kuwekeza Katika Maisha ya Watu wa Kenya: Kuthamini Manufaa ya
Uhusiano Kati ya Marekani na KenyaSura ya Nne (Sehemu ya 2 ya 3)
Kilichogunduliwa 14: Msaada wa Marekani unaolenga sekta ya utawala husaidia Kenya
kubuni vishawishi vinavyofaa ili maafisa wake waliochaguliwa
waboreshe jinsi wanavyotoa huduma na kushughulikia mahitaji ya
wananchi.
Ruwaza ya Kenya ya 2030 inatoa wito kwa nchi hiyo “kusonga mbele
kwa umoja” na kushinda historia ya utengano wa kisiasa na
mapendeleo ya kikabila na kidini wakati ambapo huduma zinatolewa
(Masakhalia, 2011; Wanjobi, 2014). Chini ya uongozi wa Rais Uhuru
Kenyatta, Kenya imejitolea kuhakikisha kwamba uwakilishi
unahusisha sauti za watu mbalimbali (k.m., misimamo mbalimbali ya
kisiasa, makabila mbalimbali) wakati wa kufanya maamuzi,
kuimarisha asasi za kiraia, kuimarisha uwazi, na kufanikisha
majadiliano mazuri ya kisiasa, miongoni mwa mambo mengine.
Marekani na Kenya zinaunganishwa na nia moja ya kuchangia katika
utawala bora na kuimarisha taasisi za kidemokrasia ambazo
zinahusisha Wakenya wote. Katika kipindi cha miongo miwili
iliyopita, serikali ya Marekani imetekeleza mipango 37 ya msaada
wa kiufundi na kuelekeza zaidi ya Dola milioni 257 kwenye shughuli
zinazounga mkono na kuimarisha mifumo ya utawala bora nchini Kenya
(tazama
Mchoro wa 15). Kati ya 2014 na 2018, Marekani ilielekeza takriban Dola
milioni 19.6 kila mwaka katika shughuli za demokrasia, haki za
kibinadamu, na utawala.
Mchoro wa 15. Msaada wa demokrasia, utawala bora na haki za kibinadamu,
uliotolewa kwa Kenya na serikali ya Marekani, 2001-2018
↩
Maelezo: Grafu hii inaonyesha pesa zilizotolewa kwa Kenya
kupitia msaada rasmi wa maendeleowa Marekani zilizoelekeza
katikademokrasia, utawala bora na haki za kibinadamu kati ya
mwaka wa 2001 na 2018 kwa msingi wa thamani isiyobadilika ya
Dola ya 2019.
Asili: USAID Foreign Aid Explorer Data.
Shughuli za kukuza utawala bora, kwa kawaida, huchukua miaka mingi
kuzaa matunda, lakini Kenya tayari imeshapiga hatua muhimu katika
suala hilo. Kenya imetoa nafasi kwa idadi inayoongezeka ya sauti
mbalimbali za kisiasa Katika miaka ya nyuma, nchi hiyo ilikuwa
nchi yenye chama kimoja (1982-1991), lakini Wakenya waliunda vyama
17 vipya vya kisiasa kati ya mwaka wa 2000 na 2009, na zaidi ya
vyama 14 vimesajiliwa kuanzia 2010 hadi sasa. Kwa sasa, wananchi
wamekuwa na fursa nzuri zaidi ya kuhakikisha sauti zao zinasikika
katika debe la kura, kwa sababu kumekuwa na ongezeko thabiti
katika viwango vya uwezo wa kuchagua kiongozi unayemtaka katika
chaguzi zenye haki na uhuru katika mwongo mmoja uliopita. Hiyo ni
kwa mujibu wa Kielezo cha Bertelsmann cha Mabadiliko ya Kenya
(Bertelsmann Transformation Index for Kenya (BTI, 2018).
Chaguzi zenye ushindani na wawakilishi mbalimbali wa kisiasa hutoa
vishawishi bora kwa viongozi waliochaguliwa kuboresha ufikiaji wa
huduma na kushughulikia mahitaji ya wapigaji kura (Sen, A. 1999;
Mehrotra, S. 2008). Kwa hivyo, tunatarajia kuona wananchi wengi
zaidi wakiweza kufikia huduma na wakiridhika na serikali sambamba
na sauti mbalimbali za kisiasa zinazozidi kuongezeka nchini Kenya
na unedeshaji wa chaguzi huru na zenye haki.
Katika hali hiyo, ni jambo la kutia moyo sana kuona kwamba nyumba
nyingi za Kenya zinaripoti kwamba zinaweza kupata maji safi
(ongezeko la asilimia 15) na umeme (ongezeko la asilimia 40) kati
ya mwaka wa 2000 na 2017, kulingana na Benki ya Dunia (WDI, n.d.).
Wakenya pia wamezidi kuwa na matumaini kwamba serikali yao inaweza
kutoa huduma hizi muhimu na wamezidi kuamini viongozi wao wa
serikalini. Habari za hivi majuzi za utafiti wa Afrobarometer
zinasema kwamba karibu asilimia 70 ya wananchi wa Kenya wanaamini
kwamba serikali inashughulikia vizuri hitaji la umma la umeme
katika mwaka wa 2018, asilimia hiyo ikiwa imeongezeka kutoka
asilimia 45 katika mwaka wa 2008. Pia, tafiti za kubaini maoni ya
raia zinazotekelezwa kila mwaka na Gallup World Poll zinazonyesha
kwamba idadi ya wananchi ambao wana imani na serikali ya Kenya
imeongezeka, kutoka asilimia 25 katika mwaka wa 2009 hadi karibu
asilimia 70 katika mwaka wa 2019.
Kenya bado ina kazi nyingi sana ya kufanya ili kutimiza malengo
yake ya Ruwaza ya 2030. Hata hivyo, nchi hiyo imeshapiga hatua
kubwa kwa kuunda nafasi za kisiasa kupitia kuwa na vyama
mbalimbali vya kisiasa na kuendesha chaguzi huru zenye haki.
Maendeleo haya ya kisiasa pia yanaambatana na kuimarika kwa
ufikiaji wa huduma muhimu na wananchi kuzidikuwa na imani kwamba
serikali itashughulikia mahitaji yao. Kuna vitu vingi ambavyo
vinasaidia Kenya kutimiza malengo yake ya utawala bora, lakini
tunaweza kusema kwamba nchi ya Marekani imekuwa mshirika muhimu
sana Kenya inapojitahidi kutimiza malengo hayo kwa kutoa msaada
muhimu wa kifedha na kiufundi.
Kilichogunduliwa 15: Msaada wa Marekani unaolenga sekta ya kilimo huimarisha
uzalishaji katika maeneo ya mashambani ya Kenya ili kuongeza
mapato na kupunguza ukosefu wa usawa.
Kadiri Kenya inavyoazimia kuwa taifa ambalo linaendelea kwa kasi
lenye pato la kati ifikapo 2030, kuimarisha sekta yake ya kilimo
ili iwe ya kisasa kwa lengo la kuongeza mavuno ya mazao kutakuwa
ni hatua muhimu si tu katika kuhakikisha kwamba kuna chakula cha
kutosha nchini, bali pia katika kuimarisha maisha ya raia
wanaoishi mashambani. Marekani imekuwa mshirika muhimu katika
kutoa msaada wa kifedha na kiufundi kwa sekta ya kilimo ya Kenya,
kupitia mipango yake ya kutoa msaada kati ya nchi mbili na kutoa
msaada wa kimataifa (tazama
Mchoro wa 16), pamoja na kupitia mikopo midogo, ruzuku, na usaidizi wa
kiufundi kutoka kwa mashirika na watu binafsi kutoka Marekani.
Mchoro wa 16. Msaada wa Marekani kwa kilimo na mazao ya sekta ya kilimo ya
Kenya, 2008-2018
↩
Maelezo: Grafu hii inaonyesha jumla ya mazao ya sekta ya kilimo
ya Kenya kati ya 2008 na 2018 kwa msingi wa thamani
isiyobadilika ya Dola ya 2019.
Asili: World Development Indicators, the World Bank.
Karibu robo tatu ya watu wa Kenya wanategemea kilimo ili wapate
kipato chao chote au sehemu ya kipato chao (USAID Kenya, n.d.).
Kilimo pia kinaletea uchumi wa Kenya mapato makubwa sana:
kilichangia asilimia 34 ya Pato la Taifa - GDP ya nchi hiyo katika
mwaka wa 2018, asilimia hiyo ikiwa imeongezeka kutokea asilimia 22
katika mwaka wa 2008.
[29]
Hivyo, hii inaonyesha kwamba uchumi wa Kenya ni thabiti, kwani,
Pato la Taifa (GDP) la Kenya lilipata kukua kwa asillimia 5.15 kwa
wastani katika kipindi hicho.
[30]
Kwa sasa, mapato ya wastani ya kila raia yameongezeka kutoka
takriban Dola 1,050 katika mwaka wa 2008 hadi takriban Dola 1,400
katika mwaka wa 2018
[31]
na ukosefu wa usawa kimapato umepungua tangu miaka ya 1990 (Jedwali la 4). Ingawa vitu vingi vinaweza kuchangia kuongezeka kwa mapato na
kupungua kwa ukosefu wa usawa, kwa vile idadi kubwa ya Wakenya
inategemea sekta ya kilimo kwa riziki yao, hiyo inamaanisha kwamba
angalau baadhi ya maongezeko hayo yametokana na kuongezeka kwa
mazao ya kilimo na mapato mengine yanayohusiana na kilimo.
Msaada wa Marekani umesaidia Kenya kuimarisha mazao yake ya kilimo
kwa njia kadhaa muhimu. Mojawapo ya vitu ambavyo Marekani
imesisitiza katika kutoa msaada wake ni kwamba mbinu bora za
kilimo zitumiwe, ili wakulima waweze kuzalisha kiwango kikubwa cha
mavuno na kupunguza vurugu vinavyotokana na hali mbovu za anga
zisizotabirika. Hiyo huletea Kenya manufaa pande mbili kwani
wanakuwa wameimarisha uhakika wa chakula kupitia kuwepo kwa
vyakula muhimu vya kutosha—kitu ambacho kimepatiwa kipaumbele
kufuatia ukame wa Afrika Mashariki wa 2011-2012— na pia wanakuwa
wamesaidia wakulima kupunguza hatari kutokana na kupunguza hasara
za kimapato. Kitu cha pili ambacho Marekani imesisitiza katika
kutoa msaada wake ni kuwasaidia wakulima wadogo waweze kufikia
masoko ya kimataifa ya bidhaa nje. Mikataba ya biashara kama vile
AGOA imechangia mazingira mazuri kwa wakulima wa Kenya ya kuongeza
mapato yao.
Jedwali la 4: Kizigeu wiano kati ya vipimo viwili cha GINI cha Kenya cha
kupima ukosefu wa usawa wa kimapato
↩
Mwaka
GINI
1992
57.5
1994
43.1
1997
45.0
2005
46.5
2015
40.8
Maelezo: Kizigeu wiano kati ya vipimo viwili cha Gini ni kigezo
kinachotumiwa kupima kiwango cha ukosefu wa usawa wakati wa
kugawa mapato ya familia katika nchi fulani. Jedwali hili
linaripoti Kizigeu wiano kati ya vipimo viwili cha Gini cha
Kenya kuanzia 1992 hadi 2015. Vizigeu wiano kati ya vipimo
viwili vya juu vinakuwepo ikiwa kuna viwango vya juu vya ukosefu
wa usawa wa kimapato, ilihali vizigeu wiano kati ya vipimo
viwili vya chini vinaashiria viwango vya chini vya ukosefu wa
usawa.
Asili: World Development Indicators, The World Bank.