Sehemu ya 4.2 Viongozi wa Kenya wana mawazo gani kuhusu michango ya Marekani katika maendeleo ya Kenya?

Katika sehemu zilizotangulia, tulijadili jinsi ambavyo kuna ushahidi kwamba Kenya inaendelea vizuri katika kutimiza malengo muhimu ya maendeleo katika nyanja kadhaa ambapo Marekani inachangia. Hata hivyo, hatuwezi kusema kwa uhakika jinsi ambavyo michango hii inachukuliwa na viongozi wa sekta ya umma, sekta ya kibinafsi na viongozi wa asasi za kiraia ambao hubuni na kutekeleza sera za maendeleo nchini Kenya. Ili kuelewa vyema zaidi, tuliwauliza viongozi wa Kenya maswali machache mtandaoni kwa kuwachagua kwa kufuata utaratibu mahususi kutoka kwenye wakala za serikali, vyuo vikuu na washauri , mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia, washirika wa kimaendeleo ambao wanaendesha shughuli nchini Kenya, na sekta ya kibinafsi. Watu hawa 133 waliojibu maswali ya hojaji hiyo walitoa maoni yao kutokana na kazi zao kwenye sekta 14, zikiwemo afya, utawala na kilimo (tazama Mchoro wa 17). [32]

Mchoro wa 17. Waliojibu maswali ya Kura ya Maoni ya Haraka ya Kenya ya 2020 ya AidData kulingana na kundi la mdau

Vyuo vikuu, washauri au vyombo vya habari, 5.4% Sekta ya kibinafsi, 10.6% Mashirika yasiyo ya kiserikali, 14.8% Mshirika wa maendeleo, 14.9% Wakala wa serikali, 54.3%

Maelezo: jumla ya watu 133 waliojibu.

Asili: AidData’s 2020 Kenya Snap Poll.

Kilichogunduliwa 16: Viongozi wa Kenya waliichukulia Marekani kama mshirika mtendaji katika maendeleo ya nchi yao na kwamba Marekani ina mfumo mzuri sana wa maendeleo wa kuigwa.

Asilimia tisini na tano ya viongozi walioulizwa maswali waliripoti kwamba Marekani ilikuwa imejihusisha kiutendaji kwenye nyanja zao za kazi na hivyo kuchangia katika maendeleo ya Kenya. [33] Asilimia themanini na tano ya viongozi hawa waliojibu maswali walihisi kwamba Marekani ilichangia pakubwa sana katika kuisaidia Kenya kutimiza malengo yake ya maendeleo kati ya mwaka wa 2010 na 2020. [34] Viongozi wachache ambao waliripoti kwamba Marekani ilichangia kidogo au haikuchangia chochote katika maendeleo ya Kenya mara nyingi walisema kwamba pesa hazikutosha, kwamba pesa zilipeanwa chini ya masharti mengi sana, na kwamba miradi ilikuwa imetekelezwa vibaya, hizi zikiwa ndizo sababu zao za kutoa maoni hayo.[35]

Katika Sura za 2 na 3, tulionyesha kwamba kuna watendaji mbalimbali wa Marekani wanaohamasisha rasilimali na kuanzisha mashirikiano ili kufaidia maendeleo na ustawi wa Kenya. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba ingawa viongozi wa Kenya kwa jumla wanathamini mchangounaotolewa na mashirika na watu binafsi kutoka Marekani, shughuli za watendaji hao hazifahamiki kwa uwazi.

Viongozi wengi wa Kenya walioulizwa maswali walisema kwamba wakala wa serikali na mifuko ya uhisani wa kibinafsi inahusika kiutendaji katika maendeleo ya Kenya (tazama Mchoro wa 18). Kati ya wale ambao walisema kwamba serikali ya Marekani inashiriki kiutendaji katika sekta yao, ni robo tu ya waliojibu maswali ambao walisema kwamba Marekani inachangia kiwango cha chini cha fedha kila mwaka ikilinganishwa na viwango halisia vya fedha ambavyo hutolewa kwa ajili ya msaada nchini Kenya.

Mchoro wa 18. Watendaji wa Marekani wanaotoa msaada sana nchini Kenya, kulingana na viongozi wa Kenya

Watu binafsi Vyuo vikuu/ washauri Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs/CSOs) Kampuni za kibinafsi Mifuko ya Uhisani Serikali ya Marekani 97.3% 89.0 79.2 77.8 68.7 67.9

Maelezo: Grafu hii inaonyesha asilimia ya viongozi wa Kenya ambao waliripoti kwamba watendaji wa Marekani wanachangia kwa kiasi fulani au kwa kiasi kikubwa, kulingana na kikundi cha mtendaji.

Asili: AidData’s 2020 Kenya Snap Poll.

Kwa kulinganishwa, watendaji wengine wa Marekani walitajwa mara chache zaidi. Cha kushangaza ni kwamba, hata hivyo, ilipofika wakati wa kusema ikiwa taasisi na watu binafsi wa Marekani wanachangia, viongozi hao walisema ndiyo kwamba wanachangia kwa maendeleo na ustawi wa Kenya. Kwa kila mmoja ya kategoria hizi za kushiriki kwa Marekani nchini Kenya, zaidi ya asilimia sitini ya waliojibu walitaja watendaji hawo kama ambao wanachangia michango mikubwa (tazama Mchoro wa 19).

Mchoro wa 19. Watendaji wa marekani wanaochangia zaidi katika maendeleo ya Kenya, kulingana na viongozi wa Kenya

Kampuni za kibinafsi Watu binafsi Vyuo vikuu/ washauri Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs/CSOs) Mifuko ya Uhisani Serikali ya Marekani 93.4% 74.4 39.8 19.6 19.1 25.1

Maelezo: Grafu hii inaonyesha asilimia ya viongozi wa Kenya ambao waliripoti kwamba michango ya Marekani katika maendeleo ya Kenya ni mingi au mingi sana, kulingana na kiukundi cha mtendaji.

Asili: AidData’s 2020 Kenya Snap Poll.

Kwa ujumla, wakala wa serikali ya Marekani, mifuko ya uhisani wa kibinafasi na kampuni za Marekani zilitajwa kama zinazotoa michango mikubwa zaidi katika maendeleo na ustwai wa Kenya; huenda hii inaonyesha kiwango kikubwa cha pesa ambacho watendaji hawa wameweza kuchangisha na pia huenda inaonyesha kwamba wapokeaji wanapendelea mtaji kuliko misaada ya kihisani.

Zaidi ya robo ya waliojibu Kura ya Maoni ya Haraka ya Kenya ya 2020 ya AidData hawakuthamini tu michango hii ya nyuma iliyotolewa kwa ajili ya maendeleo ya Kenya, bali pia walitambua kwamba Marekani ina mfumo bora kabisa wa maendeleo ambao nchi yao inapaswa kuiga (tazama Mchoro wa 20). Wananchi wa Kenya wanaamini zaidi manufaa ya kujifunza kutokana na demokrasia huru ya Marekani. Zaidi ya asilimia 50 ya waliojibu maswali ya Afrobarometer ya 2014, utafitiunaowakilisha maoni ya familia za Kenya, walisema kwamba mfumo wa Marekani wa maendeleo ndio mfumo bora zaidi wa kufuatwa na Kenya (tazama Mchoro wa 21).

Mchoro wa 20. Maoni ya viongozi kuhusu ni mfumo gani wa maendeleo ulio bora zaidi ambao Kenya unapaswa kufuata

Afrika Kusini Hakuna nchi yoyote kati ya hizi Uchina India Uingereza Nyinginezo Marekani 28.3% 25.9 17.5 9.0 8.1 7.2 4.0

Maelezo: Grafu hii inaonyesha asilimia ya viongozi wa Kenya ambao walitambua mfumo wa maendeleo wa nchi fulani kama ulio bora wa kufuatwa na Kenya.

Asili: AidData’s 2020 Kenya Snap Poll.

Mchoro wa 21. Maoni ya wananchi kuhusu mfumo bora zaidi wa maendeleo wa kufuatwa na Kenya

Marekani Uhina Mkoloni wa nchi yako Afrika Kusini Sijui Tufuate mfumo wa nchi yetu wenyewe India Nyinginezo Hakuna nchi yoyote kati ya hizi Nchi ambayo ningechagua haipo kwenye majibu 48.5% 24.3 7.4 7.3 6.1 3.2 1.8 0.8 0.5 0.1

Maelezo: Grafu hii inaonyesha asilimia ya wananchi wa Kenya ambao walitambua mfumo wa maendeleo wa nchi fulani kama ulio bora wa kufuatwa na Kenya.

Asili: Afrobarometer Kenya Survey Round 4, 2014.