Kuwekeza Katika Maisha ya Watu wa Kenya: Kuthamini Manufaa ya
Uhusiano Kati ya Marekani na KenyaSura ya Nne (Sehemu ya 1 ya 3)
Sura ya Nne Je, ni faida gani halisia na zinazofikiriwa ambazo Kenya
inapata kutokana na ushirikiano wake na Marekani?
Kufikia hapa, tumeangazia michango ya Marekani katikamaendeleo na
ustawi wa Kenya kwa njia mahususi kabisa —dola zilizohamasishwa
kila mwaka kwa wastani kupitia baadhi ya vyanzo vya umma, vya
kibinafsi na vya watu binafsi. Hata hivyo, ushirikiano kati ya
Marekani na Kenya unahusu mengi zaidi mbali na fedha. Mwishowe,
nchi zote mbili zina nia moja ya kuona kwamba Kenya inaendelea kwa
njia halisi na kutimiza malengo yake ya kiuchumi, kijamii na
kiutawala sambamba na mpango wake wa Ruwaza ya 2030.
Katika sura hii, tunaangazia maendeleo ya Kenya katika nyanja tatu
muhimu ambapo Marekani imehusika—afya, demokrasia na utawala, na
kilimo—ili kugundua jinsi ambavyo kushirikiana na Marekani
kunaweza kuchangia katika maendeleo ambayo Wakenya wanaona katika
maisha yao ya kila siku. Pia tulitafiti viongozi wa Kenya
wanaofanya kazi katika sekta 14 na makundi 5 ya wadau ili
kukadiria jinsi ambavyo walichukulia michango ya Marekani ya
kuisaidia Kenya kutimiza malengo yake. Kura yetu ya Maoni ya
Haraka ya 2020 ya Kenya iliwaomba viongozi wa sekta ya umma, sekta
ya kibinafsi na viongozi wa asasi za kiraia watoe maoni yao kuhusu
kiwango cha ushiriki wa Marekani wanachoona katika sekta zao,
umuhimu wa michango ya Marekani katika maendeleo ya Kenya, na
mfano wa maendeleo wanayopendelea kwa ajili ya nchi yao.
Sehemu ya 4.1 Je, ni jinsi gani ushirikiano kati ya Marekani na Kenya
unafaidi raia wa Kenya katika maisha yao ya kila siku?
Ili kujibu swali hili, tunaangazia mifano mitatu tofauti kwenye
sekta ambazo Marekani imezitolea kiwango kikubwa cha usaidizi wake
wa kifedha na kiufundi katika kipindi cha miongo miwili iliyopita:
Kwanza, tunaangalia utendakazi wa Kenya katika suala la kuzuia
na kutibu HIV/UKIMWI ili kutimiza malengo yake ya kijamii na
kiafya. Sekta ya Kenya ya afya kwa ujumla, hasa jitihada zake za
kupambana na HIV/UKIMWI, kihistoria, zimevutia usaidizi mkubwa
kabisa kutoka kwa jamii nzima ya Marekani (kutoka kwa serikali
na vyanzo visivyo vya serikali).
Pili, tunaangazia utendakazi wa Kenya katika kuimarisha mifumo
yake ya kidemokrasia ili kutimiza malengo yake ya kisiasa na
kiutawala. Marekani imehamasisha msaada mkubwa wa kifedha na
kiufundi katika miaka ambayo imepita ili kuunga mkono uchaguzi
wenye ushindani na uwakilishi wa kisiasa unaohusisha watendaji
mbalimbali ili kuleta vichocheo vizuri vitakavyosababishavya
huduma za umma zitolewe ipasavyo na kwa usawa kwa watu wote wa
Kenya.
Tatu, tunaangazia utendakazi wa Kenya katika sekta ya kilimo,
ambapo washiriki mbalimbali wa Marekani, ikiwemo serikali,
wanachangia na kuhusika kupitia usaidizi wa kiufundi, mikopo
midogo midogo, na ruzuku.
Kilichogunduliwa 13: Msaada kutoka Marekani unaolenga sekta ya afya husaidia sio tu
kuokoa maisha ya watu pekee, bali pia huchangia katika
uzalishaji wa uchumi wa Kenya, kadiri watu wanavyofanya kazi kwa
muda mrefu zaidi.
Wafanyakazi wenye afya wanaofanya kazi vizuri wanahitajika ili
kutimiza ndoto ya Kenya ya muda mrefu ya kuwa taifa lenye
ushindani wa kimataifa na ustawi ifikapo 2030.Katika hali hiyo,
janga la HIV/UKIMWI ni “mojawapo ya matishio makubwa zaidi kwa
maendeleo ya kiuchumi na kijamii” (Baraza la Kitaifa la Kudhibiti
Ukimwi - National Aids Control Council, 2020). Kwa mfano, Kenya
ilishuhudia ongezeko mkubwa wa maambukizo mapya ya HIV mwishoni
mwa miaka ya 1990, na ikawa mojawapo ya nchi kadhaa za Afrika
zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa HIV.
Kufuatia idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na UKIMWI katika mwaka
wa 2004, Kenya imejiimarisha katika kuzuia vifo vinavyotokana na
ugonjwa huo (tazama
Mchoro wa 13), na imepunguza idadi ya maambukizo mapya ya HIV kwa asilimia 55
tangu 2010 (UNAIDS, 2020). Uwezo naozidi kuimarika wa Kenya katika
kufanikisha mipango ya uzuiaji na matibabu—kama vile kupeana
matibabu ya kudhibiti virusi (ART) kwa watu wengi zaidi
walioathiriwa (tazama
Mchoro wa 13), na kuwawezesha watu kupata huduma ya afya kwa bei nafuu—ni
vipengele muhimu katika mafanikio hayo.
Mchoro wa 13. Vifo vinavyotokana na UKIMWI nchini Kenya (1995-2016) na
asilimia ya watu wanaoishi na HIV wanaopokea ART
(2010-2016)
↩
Maelezo: Mstari mwekundu unaonyesha idadi inayokadiriwa ya vifo
vinavyotokana na UKIMWI nchini Kenya kati ya 1995 na 2016, na
ishara husika kwamba idadi hiyo itaendelea kupungua. Mstari wa
kijani unaonyesha asilimia inayokadiriwa ya watu wanaoishi na
HIV wanaopokea ART nchini Kenya kati ya 2010 na 2016, na ishara
husika kwamba idadi hiyo itaendelea kuongezeka.
Asili: UNAIDS 2019 Estimates.
Tunakadiria kwamba jitihada za kupambana na HIV/UKIMWI nchini
Kenya zimesaidia kuokoa zaidi ya maisha milioni moja kufikia
leo.[28]
Zaidi ya hiyo, kwa vile wastani wa umri wa kuishi wa Kenya
umeongezeka katika kipindi cha miongo miwili iliyopita—kutoka
miaka 51 katika mwaka wa 2000 hadi miaka 66 katika mwaka wa 2018
(tazama
Mchoro wa 14)—hiyo inamaanisha pia kwamba kila Mkenya amepata ongezeko la
wastani wa miaka 15 yauzalishaji wa kiuchumi.
Mchoro wa 14. Muda unaotarajiwa wa maisha kuanzia wakati wa kuzaliwa nchini
Kenya, 1995-2017
↩
Maelezo: Grafu hii inaonyesha wastani wa umri wa kuishi wa
Wakenya kuanzia wakati wa kuzaliwa kutoka 1995 hadi 2017.
Asili: World Development Indicators, The World Bank.
Ushirikiano kati ya Kenya na Marekani umesaidia sana katika
kuhamasisha rasilimali na utaalamu wa kuwasaidia wafanyakazi wa
afya walioko kwenye mstari wa mbele kufanikisha jitihada zao za
kupambana na janga la HIV/UKIMWI. Tangu 2000, serikali ya Marekani
imeelekeza msaada mkubwa wa kiufundi na fedha katika sekta ya afya
ya Kenya (tazama Mchoro wa 3). Kiwango kikubwa cha mchango huu
kimetumiwa kupambana na HIV/UKIMWI nchini Kenya na kuhakikisha
kwamba ART zinapatikana. Kwa kweli, serikali ya Marekani ndio
imetoa msaada mkubwa zaidi kati ya watoaji msaada wote wa
kimataifa kwa ajili ya matibabu na udhibiti wa HIV/UKIMWI nchini
Kenya.
Ni muhimu kutaja kwamba kwa kufanya tathmini hii hatumaanishi
kwamba tumetathmini ufanisi wa shughuli mahususi za maendeleo,
ambalo ni jambo lisiloshughulikiwa kwenye utafiti huu, na kwamba
sababu nyinginezo pia huenda zimechangia katika kupungua kwa vifo
vinavyotokana na HIV/UKIMWI nchini Kenya. Licha ya hiyo, kwa vile
ongezeko la idadi ya watu wanaopata matibabu ya ART nchini Kenya
linalingana na kuongezeka kwa msaada wa Marekani katika suala hili
na pia kupungua kwa vifo, tunaweza kusema kwamba ushirikiano kati
ya Kenya na Marekani unawaletea watu wa Kenya faida kupitia
kuboreka kwa hali ya maisha na kuongezeka kwa maendeleo ya
kiuchumi.