Tangu 2010, kampuni 85 za Marekani zimewekeza takriban jumla ya Dola bilioni 2.93 nchini Kenya kupitia uwekezaji mashambani na ununuzi wa mali halisi (badala ya kuungana na kununua au kukodi majengo/vituo vilivyopo). Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja huwa tofauti kila mwaka, lakini kampuni za Kimarekani zimezalisha takriban Dola milioni 294.2 kila mwaka kama mtaji wa uwekezaji na nafasi 1,009 mpya za kazi kila mwaka tukikadiria kuanzia mwaka wa 2015 na kuendelea ili kufaidi uchumi wa Kenya (Financial Times, n.d.). Marekani ndio nambari moja kati ya nchi zote katika kuchangia nafasi za kazi ambazo Wakenya wanafanya. Jedwali la 3 linaonyesha kampuni kumi bora zaidi za Kimarekani katika uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja kwa msingi wa wa thamani ya dola zilizowekezwa kati ya 2010 na 2019.
Jedwali la 3.
Makampuni 10 bora zaidi ya Marekani yanayowekeza nchini Kenya, 2010-2019
↩
| 1 |
Cummins |
Nishati inayoweza kutumiwa upya |
Dola |
460 |
251 |
| 2 |
Dupre Investments |
Usafirishaji na mabohari |
Dola |
398 |
216 |
| 3 |
General Electric (GE) |
Nishati inayoweza kutumiwa upya, vifaa vya matibabu, usafirishaji na mabohari |
Dola |
359 |
80 |
| 4 |
Coca-Cola |
Vyakula na vinywaji |
Dola |
243 |
2,616 |
| 5 |
IBM |
Huduma za programu na Teknolojia ya habari |
Dola |
127 |
359 |
| 6 |
Ormat Technologies |
Nishati inayoweza kutumiwa upya |
Dola |
104 |
60 |
| 7 |
Alternet Systems |
OEM ya Usafirishaji usiotegemea injini |
Dola |
73 |
1,361 |
| 8 |
Mars |
Vyakula na vinywaji |
Dola |
65 |
847 |
| 9 |
MasterCard |
Huduma za kifedha, huduma za program tumizi na teknolojia ya habari |
Dola |
62 |
91 |
| 10 |
Microsoft |
Huduma za programu na teknolojia ya habari |
USD |
55 |
83 |
Maelezo: Jedwali hili linafafanua dola za uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja na kazi za ndani ya nchi zilizochangiwa na kampuni10 kubwa zaidiza Marekani zinazoendesha shughuli zao nchini Kenya kulingana na kiasi cha uwekezaji wao. Dola za uwekezaji wa moja kwa moja ni wa mamilioni na ni kwa msingi wa thamani isiyobadilika yaDola ya 2019.
Asili: Financial Times fDi Markets database.
Nishati inayoweza kutumika upya, usafirishaji na shughuli za mabohari, na viwanda vya chakula na vinywaji vilivutia kiwango kikubwa kabisa cha mtaji wa uwekezaji wa Kimarekani, jumla yake ikiwa ni Dola bilioni 1.8 zilizowekezwa tangu 2010 (tazama Mchoro wa 10). Nafasi za kazi zilichangiwa zaidi na shughuli za utengenezaji kwenye viwanda vya vyakula na vinywaji na usafirishaji, ikifuatwa na huduma za program tumizi na teknolojia ya habari. Huku uwekezaji ukizidi kuongezeka kutoka kwa kampuni bora zaidi za teknolojia za Marekani kama vile Oracle na Microsoft, na uwekezaji wa hivi majuzi kabisa kutoka kwa Amazon na Facebook, kampuni za Kimarekani zimewekeza katika teknolojia za baadaye pamoja na shughuli za kawaida za utengenezaji.