Kuwekeza Katika Maisha ya Watu wa Kenya: Kuthamini Manufaa ya
Uhusiano Kati ya Marekani na KenyaSura ya Tatu (Sehemu ya 1 ya 2)
Sura ya TatuJe, ni jinsi gani kampuni, mashirika, na watu wa Marekani
wanachangia katika ustawi wa Kenya?
Kuna njia nyingi tofauti tofauti ambazo Marekani inatumia
kushirikiana na Kenya. Kwenye sura iliyotangulia, tuliangazia
misaada ya serikali ya Marekani. Kwenye sura hii, tunaangazia
michango ya Marekani kutoka kwenye jamii yake kwa ujumla—kuanzia
kampuni ambazo zinahamasisha utoaji wa mtaji kwa ajili ya sekta ya
kibinafsi na watekelezaji wa mpango wa kuchangisha fedha kutoka
kwa mifuko ya misaada ya kibinafsi, hadi mashirika yasiyo ya
kiserikali yanayofadhili maendeleo ya jamii mashinani pamoja na
watu binafsi kupata mapato ambayo yanaimarisha maisha yao.
Tukijumlisha zote, tunakadiria kwamba usaidizi kutoka kwenye
kampuni, mashirika na watu binafsi wa Marekani, huchangia takriban
Dola bilioni 1.36 kila mwaka kwa uchumi wa Kenya. Michango hii ya
kila mwaka inajumuisha takriban: Dola milioni 87.3 kutoka kwenye
mifuko ya uhisani wa kibinafsi, Dola milioni 4.6 kwa ajili ya
mikopo midogo midogo na michango ya watu binafsi, Dola milioni 270
kwa ajili ya shughuli za NGO, Dola milioni 294.2 kwa ajili ya
uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja wa, Dola milioni 190.7
zilizotokana na utalii, na Dola milioni 517.6 zilizotumwa kutoka
ng’ambo na Wakenya wanaofanya kazi nchini Marekani. Kwenye sehemu
iliyobaki ya sura hii, tunazungumzia kila mmoja ya njia hizi ili
kuelewa ni jinsi gani zinawasaidia Wakenya.
Sehemu ya 3.1Uhisani wa kibinafsi kutoka Marekani na msaada kutoka kwa watu
kuelekea kwa watu uliotolewa kwa nchi ya Kenya
Mifuko ya uhisani wa kibinafsi ya Marekani na watu binafsi ni
washirika wanaozidi kuwa muhimu sana katika kufanikisha jitihada
za Kenya za kuleta maendeleo na ujasiriamali. Mashirika ya hisani
huhamasisha fedha kwenye sekta ya kibinafsi ili kufadhili miradi
ya maendeleo ya mashinani, pamoja na kutoa msaada muhimu sana kwa
mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia zinazoendesha shughuli
zao nchini Kenya. Kwa upande mwingine, kuimarika kwa teknolojia za
habari na mawasiliano kumezidisha mawasiliano na ushirikiano kati
ya Wamarekani na wenzao walioko nchini Kenya. Katika sehemu hii,
tunaangazia jinsi ambavyo mashirika ya hisani ya kibinafsi ya
Marekani na usaidizi unaotoka kwa mtu mmoja hadi mwingine
yanasaidia Kenya kutimiza malengo yake ya ustawi na maendeleo
yanayoambatana na Ruwaza ya 2030.
Kilichogunduliwa 7: Mifuko saba mikubwa zaidi ya uhisani wa kibinafsi ya Marekani
ilifadhili shughuli za maendeleo zenye thamani ya takriban Dola
milioni 87.3 kila mwaka, huku ikitilia mkazo sekta za afya,
uhakika wa chakula, na utawala bora.
Wahisani wa Marekani ni pamoja na wafadhili saba wa kibinafsi
wakubwa zaidi ulimwenguni yaani: Mfuko wa Uhisani wa Arcus (the
Arcus Foundation), Mfuko wa Uhisani wa Bill & Melinda (the Bill &
Melinda Gates Foundation), Mfuko wa Uhisani wa Conrad N. Hilton
(the Conrad N. Hilton Foundation), Mfuko wa Uhisani wa David &
Lucile Packard (the David & Lucile Packard Foundation), Mfuko wa
Uhisani wa Ford (the Ford Foundation), Mfuko wa Uhisani wa John D.
& Catherine T. MacArthur (John D. & Catherine T. MacArthur
Foundation), na Mfuko wa Uhisani wa William & Flora Hewlett (the
William & Flora Hewlett Foundation). Kwa pamoja, mifuko hii saba
ya uhisani ya Kimarekani ilitoa takriban Dola milioni 87.3[22]kwa mwaka kuanzia 2014 hadi 2018 ili kufadhili shughuli za
maendeleo nchini Kenya.[23]
Hii inajumuisha Dola milioni 76.2 zilizopeanwa moja kwa moja ili
kufadhili mashirika ya ndani ya nchi na ya kimataifa yanayoendesha
shughuli zao nchini Kenya, pamoja na takriban Dola milioni 11.1
zilizotolewa na Mfuko wa Uhisani wa Bill & Melinda Gates (the Bill
& Melinda Gates Foundation) kupitia ufadhili wake kwa Ushirika wa
Kimataifa wa Chanjo (Global Alliance for Vaccines, GAVI), Hazina
ya Dunia (Global Fund), na Shirika la Afya Duniani (World Health
Organization, WHO).
Katika mwaka wa 2018, asilimia 57 ya ufadhili wote kutoka kwa
wahisani hawa saba wa Marekani ulielekezwa katika kukuza afya bora
na halibora ya raia wa Kenya, kuimarisha shughuli za kilimo, na
kuboresha uhakika wa chakula kwa ujumla. Asilimia 11 ya fedha hizi
za msaada zilielekezwa katika miradi inayoendeleza jitihada za
Kenya za kuimarisha utawala wake na haki za kibinadamu.
Kilichogunduliwa 8: Raia binafsi wa Marekani walihamasisha takriban Dola milioni
4.6 kila mwaka kupitia michango ya kibinafsi na mikopo yenye
riba ya chini au isiyokuwa na riba kwa ajili ya kusaidia miradi
ya maendeleo nchini Kenya. Fedha hizo zilihamasishwa kwa kutumia
majukwa matatu ya kuchangisha fedha mtandaoni kupitia vikundi
vikubwa vya watu.
Katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita, majukwaa ya kuchangisha
pesa kutoka kwa vikundi vikubwa vya watu mitandaoni yameongezeka
sana. Majukwaa hayo yanawezesha msaada kutoka kwa mtu mmoja hadi
mwingine kwa njia mbili—michango na mikopo midogo.
GlobalGiving—ni jukwaa la kuchangishia pesa kutoka kwa vikundi
vikubwa vya watu mitandaoni ambalo hukagua na kuwezesha michango
kwa ajili ya mashirika ya kijamii ya ndani ya nchi —jukwaa hili
linaripoti kwamba asilimia 77 ya zaidi ya Dola milioni 5.6
zilizochangishwa kwa ajili ya miradi ya Kenya na watu binafsi kati
ya 2004 na 2019 zilitoka kwa wafadhili wa kutoka marekani. Katika
miaka mitano iliyopita, Wakenya walipokea jumla ya michango ya
Dola 383,000 kwa mwaka kwa wastani kutoka kwa Wamarekani kupitia
GlobalGiving.[24]
Michango hii ilifadhili mamia ya miradi katika sekta mbalimbali
zikiwemo sekta ya elimu, maendeleo ya kiuchumi na biashara na afya
(tazama
Mchoro wa 9).
Mchoro wa 9. Jumla ya michango yote kwa Kenya kutoka kwa watoaji misaada
binafsi wa Kimarekani kulingana na kategoria ya mradi kwenye
jukwaa la GlobalGiving, 2004-2019
↩
Maelezo: “Watoto” ni sekta inayohusiana na sekta hizo nyingine
kama ilivyofafanuliwa na GlobalGiving. Miradi iliyopo kwenye
kategoria ya “watoto” inaambatana na sekta za Usawa wa kijinsia
& kuwawezesha wanawake, elimu na afya. Kiwango cha juu cha
misaada kwenye miradi iliyoko katika sekta hii kinaonyesha
motisha ya wafadhili katika ufadhili wa watu kibinafsi.Viwango
vya pesa vilivyoonyeshwa ni kwa msingi wa thamani isiyobadilika
ya dola ya 2019.
Asili: GlobalGiving.
Majukwaa yanayopeana mikopo midogo kama vile Kiva na Zidisha,
yanayounganisha wakopeshaji na wakopaji binafsi wanaohitaji mtaji,
yameanza kutumiwa na watu wengi zaidi katika miaka ya hivi majuzi.
Wakopaji mara nyingi huwa wanaishi katika maeneo ya mashambani
ambapo hapana miundombinu mizuri ya kifedha au ni watu ambao
hawawezi kupata mikopo ya kawaida kutokana na vikwazo vingi
vilivyopo vya kuomba mikopo. Majukwaa haya yanayopeana mikopo
midogo dogo husaidia sana biashara nyingi ndogo ndogo za Kenya na
wajasiriamali binafsi kupata mtaji kupitia mikopo yenye riba ya
chini.
Kiva ni mojawapo ya majukwaa makubwa kabisa yanayopeana mikopo
midogo midogo, huku ikiwa na wakopaji zaidi ya milioni 3.6 katika
nchi 76, ikiwemo Kenya. Kwa upande wa Kiva, wakopeshaji binafsi
ambao wametambuliwa kuwa wa Kimarekani walitaja kwamba Dola
milioni 3.6 zilipeanwa kama mikopo midogo kwa Kenya kwa mwaka
kuanzia 2014 hadi 2018. Kiwango hiki, hata hivyo, ni kiwango
kidogo kwani jumla ya michango kutoka kwa watumiaji Wamarekani ni
nyingi zaidi, kwa vile karibu nusu ya watumiaji wa Kiva huwa
hawataji nchi yao asilia wanapofungua akaunti zao. Mikopo mingi
zaidi ya Kiva ambayo Kenya ilipokea ilifadhili biashara za kilimo
na vyama vya ushirika vya kilimo vya ndani ya nchi kama vile
kikundi cha Ann, chama cha ushirika cha wakulima tisa wadogo.
Zidisha ni mfano wa jukwaa dogo zaidi, linalopeana mikopo midogo
midogo linaloendesha shughuli zake katika nchi tano tu: Kenya,
Ghana, Indonesia, Nigeria, na Zambia. Watumiaji Wamarekani wametoa
mikopo ya kiwango wastani cha Dola 611,000 kwa mwaka
[25]
katika mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali Wakenya kupitia
jukwaa la Zidisha.
Kati ya majukwaa haya mawili, Kiva na Zidisha, watumiaji
Wamarekani walitoa moja kwa moja mikopo ya kiwango wastani cha
Dola milioni 4.2 kwa mwaka kwa Wakenya,
[26]
katika mikopo yenye riba ya chini au isiyo na riba ili kuwasaidia
watu waanzishe na waendeleze biashara ndogo ndogo katika nchi ya
Kenya.
Sehemu ya 3.2 Mashirikia ya Marekani yasiyo ya kiserikali yanayoendesha
shughuli zao nchini Kenya
The United States is home to approximately 1.5 million
non-governmental organizations (NGOs), many of which are actively
engaged in supporting overseas development activities. U.S.-based
NGOs add value for the Kenyan people in a variety of ways—from
direct service delivery and education to advocacy and research. In
this section, we examine how U.S. non-governmental organizations
active in Kenya are improving livelihoods in line with Kenya’s
Vision 2030.
Kilichogunduliwa 9: Zaidi ya Mashirika 1,000 yasiyo ya kiserikali ya Marekani
yanayoendesha shughuli zao nchini yalitoa takriban Dola milioni
270 kwa mwaka kwa uchumi wa Kenya, bila kujumuisha misaada kati
ya nchi mbili.
Beyond direct giving and microfinance, over 1,000 U.S.-based
non-governmental organizations (as of 2017) were actively
implementing community-based development projects in Kenya. These
non-profit organizations range in scale from small community-based
organizations with budgets in the thousands of dollars to
organizations with multinational operations and budgets in the
hundreds of millions, such as the International Rescue Committee
(IRC).
Using tax-filing information for the 2017 tax year from a database
of registered U.S. nonprofits, we estimate that over 1,000
U.S.-based NGOs contributed nearly USD 270 million in 2017 to the
Kenyan economy through their activities. This amount excludes USD
42 million of U.S. government grants given to these NGOs to
implement development projects, as these are already counted in
the bilateral aid flows.
[27]