Sura ya Kwanza
Utangulizi
Kenya inaazimia kuwa "taifa lenye ushindani na ustawi wa viwango
vya kimataifa na lenye kiwango cha juu cha ubora wa maisha ifikapo
mwaka wa 2030" (Mpango wa Kwanza wa Muda wa Kati, 2008-2012). Ili
kufanikisha maono hayo ya kiwango cha juu, Kenya lazima iendeleze
miundombinu yake ili iwe ya kisasa, iongeze utengenezaji wa bidhaa
na mauzo ya nje, na ifuate mifumo mwafaka ya utawala ili
kuhakikisha kuwa raia wote wananufaika kutokana na maendeleo ya
kiuchumi ya Kenya.[1]
Ushirikiano wa kimkakati na marafiki kama Marekani ni muhimu
katika jitihada za Kenya za kufikia Ruwaza yake ya 2030. Kwa zaidi
ya miaka 50[2], serikali ya Marekani imewekeza katika watu na taasisi za Kenya,
ikishirikiana na umma, asasi za kiraia, na watendaji wa sekta ya
kibinafsi. Licha ya hiyo, michango ya Marekani katika maendeleo ya
Kenya ni zaidi ya msaada kutoka kwa serikali ya Marekani pekee.
Kampuni za Marekani, vyuo vikuu, mashirika ya hisani, mashirika
yasio ya kiserikali (NGOs), na watu binafsi wamezidi kushirikiana
na wenzao nchini Kenya kwa miongo kadhaa iliyopita.
Licha ya uhusiano huu wa muda mrefu, viongozi wa Kenya na umma
hawawezi kupata taarifa kwa urahisi ili kutathmini thamani ya
ushirikiano wa nchi yao na Marekani.[3]
Ingawa ni vigumu kuonyesha manufaa yote ambayo Kenya imepata
kutokana na uhusiano wake na Marekani, ripoti hii inatoa makadirio
ya kihafidhina ya michango ya Marekani katika ukuaji na ustawi wa
Kenya, ikiwemo michango kutoka kwa watendaji wa kiserikali na
wasio wa kiserikali. Kwa kiwango cha chini, tunakadiria michango
hiyo kwa jumla kuwa takriban Dola bilioni 3.05 kila mwaka, kwa
wastani (tazama
Jedwali la 1).
Katika sura ya pili, tunatathmni takriban Dola bilioni 1 kwa mwaka
kwa wastani katika michango ya moja kwa moja kutoka kwa serikali
ya Marekani ili kusaidia mpango wa Ruwaza ya 2030 ya serikali ya
Kenya. Pia tunatathmini wastani wa takriban Dola milioni 678 kwa
mwaka ambayo serikali ya Marekani imehamasisha kwa njia isiyo ya
moja kwa moja kupitia sera na taasisi za ndani zinazofaidi Kenya.
Katika sura ya tatu, tunahesabu takriban Dola bilioni 1.36 kwa
wastani kwa mwaka katika michango kutoka kwa watu, mashirika, na
kampuni za Marekani katika ustawi wa Kenya. Michango hii ni ya
aina mbalimbali, kuanzia vitendo vya watu binafsi (k.m. utalii,
fedha zinazotumwa nchini Kenya, michango ya kibinafsi) hadi juhudi
za kitaasisi zaidi (k.m., misaada kutoka kwa mashirika ya ufadhili
ya Marekani, shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali ya
Marekani, uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja).
Katika sura ya nne, tunachambua matokeo ya utafiti wa AidData 2020
wa viongozi wa Kenya wa sekta ya umma na ya kibinafsi pamoja na
viongozi wa asasi za kiraia ili kuelewa jinsi wanavyotathmini
ushirika wa nchi yao na Marekani. Pia tutatathmini manufaa za
kiuchumi, kijamii na za kiutawala zinazoweza kupatikana katika
siku za usoni kutokana na shughuli za Marekani nchini Kenya.
Tunatamatisha katika sura ya tano kwa kurudia kimuhtasari mambo
makuu ya kutia akilini kutoka kwa utafiti huu.
Jedwali la 1.
Muhtasari wa makadirio ya kila mwaka ya michango ya Marekani
katika ukuaji na ustawi wa Kenya, mamilioni ya Dola/KSH
↩
Msaada kati ya nchi mbili |
Dola |
931.0 |
Ksh |
94,721.3 |
Msaada wa kimataifa |
Dola |
73.5 |
Ksh |
7,473.3 |
Michango ya Marekani ya Moja kwa Moja
|
Dola |
1,004.5 |
Ksh |
102,194.6 |
Biashara |
Dola |
576.2 |
Ksh |
58,622.6 |
Dhamana za uwekezaji |
Dola |
82.4 |
Ksh |
8,387.1 |
Msaada wa masomo |
Dola |
19.6 |
Ksh |
1,994.1 |
Faida za sera za Marekani |
Dola |
678.2 |
Ksh |
69,003.8 |
Michango ya serikali ya Marekani
|
Dola |
1,682.7 |
Ksh |
171,198.4 |
Fedha zilizotumwa nchini Kenya
|
Dola |
517.6 |
Ksh |
52,660.2 |
Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja
|
Dola |
294.2 |
Ksh |
29,931.7 |
Shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali ya Marekani
|
Dola |
270.0 |
Ksh |
27,469.8 |
Utalii |
Dola |
190.7 |
Ksh |
19,406.7 |
Michango ya Hisani |
Dola |
87.3 |
Ksh |
8,882.0 |
Mikopo midogo |
Dola |
4.2 |
Ksh |
427.3 |
Michango ya kibinafsi |
Dola |
0.4 |
Ksh |
39.0 |
Michango ya jamii ya Marekani
|
Dola |
1,364.4 |
Ksh |
138,816.7 |
Jumla ya Michango ya Marekani
|
Dola |
3,047.1 |
Ksh |
310,015.1 |
Maelezo: Jedwali hili linaonyesha wastani wa michango kutoka
Marekani katika ukuaji na ustawi wa Kenya kwa msingi wa thamani
isiyobadilika ya Dola ya mwaka wa 2019 kwa kila kategoria.
Tulipiga hesabu ya kadirio la mchango wa kila mwaka kwa kila
aina ya msaada kwa kuchukua wastani wa miaka yote ya data
inayopatikana kati ya mwaka wa 2014 na 2018, ila hatukuzingatia
masuala yote. Idadi ya miaka iliyotumiwa kupiga hesabu ya
wastani ilibadilika kulingana na idadi ya miaka iliyopatikana
katika asili ya data. Kiwango cha ubadilishaji wa sarafu cha
Dola 1 = 101.74 KSH kilitumiwa.
Asili: Makadirio ya AidData. Tazama Kiambatisho cha Kiufundi
kinachoambatana na ripoti hii kwa maelezo zaidi.