← Kuhusu ripoti
Cover image of the report Investing in Tanania's People.

Kuwekeza kwa Watu wa Tanzania:

Kuthamini Ushirikiano wa Marekani na Tanzania kwa Maendeleo

Mei 2024

Divya Mathew, Bryan Burgess, Samantha Custer, Rodney Knight, Kelsey Marshall, Lucas Katera, Jane Mpapalika, Constantine George Simba na Cornel Jahari

Muhtasari Mahsusi

Nchi ya Marekani ni mshirika mkuu wa Tanzania. Uhusiano kati ya nchi hizi mbili umejengwa katika mihimili mitatu: diplomasia, maendeleo na ulinzi. Hata hivyo, kuna taarifa chache zinazopatikana kwa Watanzania kwa urahisi ili kuwawezesha kutathmini thamani ya ushirikiano huo katika maisha yao ya kila siku, hasa wanapopima maendeleo ya kufikia malengo ambayo nchi imejiwekea katika Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025. Ripoti hii inabainisha jinsi ambavyo ushirikiano wa Marekani na Tanzania unachangia ukuaji na mafanikio ya Tanzania—kupitia rasilimali zinazokusanywa na matokeo yanayotokana na rasilimali hizo.

Watafiti wamezingatia maoni ya jamii nzima kwa kuchunguza sio tu msaada rasmi wa maendeleo bali pia michango ya sekta binafsi kupitia biashara, utalii, uwekezaji, hisani, na miamala mbalimbali. Utafiti huu unachanganua historia ya mtiririko wa fedha kutoka vyanzo vya Marekani kwenda Tanzania kwa takriban muongo mmoja, kuanzia 2012 hadi 2022. Pia, utafiti unahusisha maoni ya viongozi wa umma, sekta binafsi na mashirika ya kiraia jinsi wanavyotathmini ushirikiano huo kwa sasa kupitia dodoso na usaili. Uchambuzi wa data ulifanywa na AidData- Maabara ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafti ya William & Mary ya nchini Marekani kwa ushirikiano na REPOA- Shirika la Utafiti wa Sera Tanzania.

Kuhusiana na fedha, mashirika ya serikali ya Marekani, kampuni na watu binafsi kwa pamoja huchangia takribani dola bilioni 2.8 kila mwaka (TZS Bn 7,140) kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania. Serikali ya Marekani inachangia takribani dola bilioni 1.0 kila mwaka (TZS Bn 2,550), katika sekta ya afya, kilimo na miundombinu. Mnamo 2022, hii ni pamoja na misaada ya moja kwa moja ya makubaliano ya nchi na nchi na misaada ya kimataifa (USD milioni 824.2) na mchango wa sera za biashara na uwekezaji (USD milioni 205.3). Vyanzo vya Marekani ambavyo si vya wakala wa serikali vinachangia takribani dola bilioni 1.8 kila mwaka (TZS Bn 4,590) kupitia uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja (USD bilioni 1.3), fedha kutoka kwa Watanzania wanaofanya kazi Marekani (USD milioni 103.7), mapato ya utalii (USD milioni 317.7), na mashirika binafsi (USD milioni 96.3), pamoja na michango ya mtu mmojammoja na mikopo midogomidogo (USD milioni 0.3). Pamoja na manufaa hayo ya kifedha, ushirikiano wa Marekani na Tanzania unachangia ukuaji na ustawi wa jamii kwa njia mbalimbali:

Sura ya 1: Utangulizi

Tanzania imejiwekea lengo madhubuti la kuongeza ushindani wake wa kiuchumi na kuimarisha msingi wa viwanda ifikapo 2025 kwa namna inayochochea maendeleo ya watu wake (Dira ya Taifa ya Maendeleo Tanzania 2025). Katika hali halisi, Serikali ya Tanzania inachukulia kwamba kuongeza ufanisi na tija ya viwanda kuwa muhimu katika kufikia dira yake kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa wingi ndani ya nchi.

Ushirikiano wa Tanzania na Marekani pamoja na washirika wengine wa maendeleo una nafasi kubwa katika kufanikisha jitihada za Tanzania kufikia Dira ya 2025. Ukweli huo upo thabiti kwa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amesisitiza kwamba "kujitegemea kunatokana na juhudi na uwezo wetu wa nyumbani," Hata hivyo, Tanzania lazima "ijifunze kwa dhati mifano ya mafanikio kutoka nje ya nchi, ili kufikia maendeleo tunayomaanisha na kuyatafuta” (Maelezo ya utangulizi, FYDP III).

Tangu kupata uhuru wake 1961, Tanzania imedumisha uhusiano wa kidiplomasia na Marekani na kushirikiana katika mipango ya kiuchumi na maendeleo kwenye sekta mbalimbali. Serikali ya Marekani imewekeza kwa raia na taasisi za Tanzania, ikishirikiana na serikali, mashirika ya kiraia na wadau wa sekta binafsi katika maeneo ya afya, miundombinu, elimu, mazingira na utawala, miongoni mwa maeneo mengine. Makampuni ya Marekani, vyuo vikuu, mashirika ya misaada, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), na watu binafsi wameendelea kushirikiana na raia wa Tanzania kwa miongo kadhaa iliyopita. Licha ya ushirikiano huo kudumu muda mrefu, viongozi wa nchi zote mbili hawana taarifa zinazopatikana kwa urahisi ili kutathmini thamani ya ushirikiano wao.[1]

Ushirikiano wa Marekani na Tanzania si kwamba hauna mapungufu, Washington na Dodoma zinatofautiana kuhusu masuala kadhaa yakiwemo rushwa, haki za binadamu, na taratibu za uchaguzi (Gavin, 2022; Wilson Center, 2022). Kwa mfano: Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani (MCC) lilisimamisha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 2016, kabla ya kuzirejesha kwa mkataba wa masharti makubwa 2023 (Cooke na Huber, 2016; Afrika Mashariki, 2023). Pia, Marekani si mdau pekee anayesaidia ukuaji na mafanikio ya Tanzania, kwa kuwa Tanzania imekuza uhusiano wa karibu na wafadhili wengine wa Kaskazini na washirika wa Kusini-Kusini kama vile Jamhuri ya Watu wa China (PRC). Hata hivyo, ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania umedumu kwa zaidi ya miaka 60 na umeendelea kuwa msingi imara katika kuisaidia Tanzania kufikia malengo ya maendeleo kwa mujibu wa Dira yake 2025.

Katika ripoti hii, tunatumia maoni ya jamii nzima katika kukadiria sio tu msaada rasmi wa maendeleo kutoka Serikali ya Marekani bali pia michango ya sekta binafsi kupitia biashara, utalii, uwekezaji, uhisani na miamala. Kwa kifupi, tunakadiria jumla ya mchango huo kufikia takribani dola bilioni 2.8 kila mwaka (TZS 7,140 Bn), kwa wastani ( Tazama Jedwali Na. 1). Utafiti huu unachambua mtiririko wa fedha kihistoria kutoka vyanzo vya Marekani kwenda Tanzania kwa takribani muongo mmoja uliopita.[2] Pia, unahusisha uelewa wa viongozi wa umma, watu binafsi na mashirika ya kiraia jinsi wanavyotathmini ushirikiano huo kwa sasa kwa kutumia dodoso na usaili. Uchambuzi wa data ulitolewa na AidData- Maabara ya Kimataifa ya Taasisi ya Utafiti ya William & Mary ya nchini Marekani, kwa ushirikiano na REPOA- Shirika la Utafiti wa Sera Tanzania.

Katika Sura ya 2 na 3, tunaonesha mtiririko wa fedha ili kubainisha nafasi ya Serikali na Sekta binafsi ya Marekani katika kusaidia ukuaji na ustawi wa Tanzania. Pamoja na kusimamishwa kwa shughuli za MCC kwa muda, Serikali ya Marekani ilichangia takribani dola bilioni 1.0 kila mwaka (TZS Bn 2,550). Mnamo 2022, hii ni pamoja na misaada ya moja kwa moja (USD milioni 824.2) na nyongeza ya dola milioni 205.3 kutokana na thamani iliyokusanywa kwa kutumia Sera za ndani za Marekani zinazonufaisha uchumi wa Tanzania. Bila shaka, ushirikiano wa Marekani na Tanzania ni zaidi ya mwingiliano kati ya Serikali na Serikali.

Kwa kuzingatia nafasi ya watu binafsi, makampuni na mashirika, tunakadiria kuwa mwingiliano wa watu unazalisha wastani wa dola za Kimarekani bilioni 1.8 kwa mwaka (TZS Bn 4,590),kama rasilimali za ziada zinazoweza kuchangia mafanikio ya Tanzania. Michango hii hudhihirika kwa namna mbalimbali, kuanzia shughuli za watu binafsi (k.m., utalii, fedha zinazotumwa kutoka Marekani, michango ya watu binafsi) hadi juhudi za kitaasisi (k.m., ruzuku kutoka mashirika ya misaada yenye makao yake makuu nchini Marekani na uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja).

Katika Sura ya 4, tunatathmini ikiwa michango ya kifedha ya Marekani inatafsiri manufaa yanayopatikana kwa faida na ustawi wa watu wa Tanzania. Tunachambua matokeo ya utafiti wa 2024 na mfululizo wa usaili kuhusu usuli wa viongozi wa umma wa Tanzania, sekta binafsi na mashirika ya kiraia juu ya maoni yao kuhusu kiwango cha mafanikio ya ushirikiano wa Tanzania na Marekani. Pia tunaunganisha na vyanzo vya data za maktabani kueleza uwezekano uliopo wa faida ya kiuchumi, kijamii na utawala bora katika ushiriki wa Marekani nchini Tanzania. Tunahitimisha katika Sura ya 5 kwa kuangazia kwa muhtasari mafunzo makuu yanayotokana na utafiti huu.

Jedwali Na. 1. Mchanganuo wa makadirio ya michango ya kila mwaka ya Marekani katika ukuaji na mafanikio ya Tanzania kwa mamilioni ya USD na TZS.

2012-2022, Jumla Milioni za USD 2022 Thamani,
Milioni za USD
2012-2022, Jumla,
Bilioni za TZS
Jumla ya Serikali ya Marekani na Jamii 31,381.9 3,006.9 80,023.9
Makubaliano ya nchi na nchi 7,402.3 499.5 18,875.9
Makubaliano ya Kimataifa 2,299.5 324.7 5,863.7
Mchango wa Marekani wa moja kwa moja 9,701.8 824.2 24,739.6
Biashara (za nje) 1,490 170.90 3,799.5
Dhamana za uwekezaji 93.3 30.8 237.9
Ufadhili wa masomo 37.1 4.5 94.6
Faida ya Sera za Marekani 1,615.4 205.3 4,119.3
Jumla ya Mchango wa Serikali ya Marekani 11,317.2 1,029.5 28,858.9
Miamala* 1,141.2 148.6 2,910.1
Uwekezaji wa nje wa moja kwa moja 14,365.7 1,403 36,632.5
Utalii 3,495 327.5 8.912.2
Michango ya Hisani 1,059.2 98 2,701
Mikopo midogomidogo* 3.6 0.3 9.2
Jumla ya Michango Jamii ya Marekani 20,064.7 1,977.4 51,165
Dokezo: Jedwali hili linaonyesha wastani wa michango inayotokana na Marekani katika ukuaji na ustawi wa Tanzania kwa kikategoria (USD 2022 kwa mfululizo). Tulitumia data ya 2022 za mwaka wa hivi karibuni zaidi, isipokuwa pale ambapo data haikupatikana na ilitubidi kutoa makadirio (yaliyoonyeshwa na nyota). Idadi ya miaka iliyotumika kupata wastani ilitofautiana kulingana na miaka iliyotumika katika chanzo cha data. Kigezo cha ubadilishaji cha Dola 1 = 2550.00 TZS kilitumika. Chanzo: makadirio ya AidData. Tazama kiambatisho cha kitaalam kwa maelezo zaidi.

Sura ya 2: Serikali ya Marekani inachangiaje mafanikio ya Tanzania?

Mnamo mwaka 2023, Serikali za Marekani na Tanzania ziliadhimisha miaka 62 ya uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kimaendeleo. Washington na Dodoma ziko tayari kuendeleza uhusiano huo katika siku za usoni. Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, alitoa msaada wa dola za Marekani milioni 560 mwaka 2024 kwa makubalinao ya nchi hizo mbili wakati wa ziara yake ya Aprili 2023 kwa Rais Samia Suluhu Hassan (Ubalozi wa Marekani - Italia, n.d.). MCC mwezi Desemba 2023 ilitangaza kwamba Tanzania imechaguliwa kwa mkataba wa programu ya ruzuku ndogo ya kusaidia mageuzi ya kuondoa vikwazo vya ukuaji wa uchumi. MCC kwa kushauriana na Wizara ya Fedha na Tume ya Mipango ya Tanzania, kwa pamoja imeteua sekta zinazolengwa katika mpango huo mpya (MCC, Februari 2024).

Serikali ya Marekani inaunga mkono ukuaji na ustawi wa Tanzania kwa njia tatu: (1) makubaliano ya msaada kwa nchi na nchi, (2) Msaada wa kimataifa, na (3) kuweka mazingira mazuri ya kisera ili kuwezesha biashara, uhamiaji na uwekezaji. Kwa jumla, tunakadiria kwamba msaada unaotolewa na Serikali ya Marekani huchangia takribani dola bilioni 1.0 kwa mwaka katika uchumi wa Tanzania. Mnamo 2022, hii ni pamoja dola milioni 824.2 (TZS Bn 2,550) za misaada ya moja kwa moja ya makubaliano ya nchi na nchi. Pia, inahusisha Dola za Marekani milioni 205.3 katika michango inayotokana na mazingira ya sera nzuri za Marekani. Katika sura hii, tunachunguza njia hizo tatu ili kubainisha jinsi zinavyochangia thamani ya maisha ya watu wa Tanzania.

2.1 Mchango wa moja kwa moja wa Serikali ya Marekani kwa Tanzania

Fedha za maendeleo za serikali ni njia muhimu ya msaada wa Serikali ya Marekani katika ukuaji, ustawi na utulivu wa Tanzania. Hii ni pamoja na misaada, mikopo isiyo na riba au yenye riba nafuu, msaada usio wa kifedha na wa kiufundi pamoja na mikopo inayowiana na viwango vya soko na mauzo ya nje (deni). Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, Marekani imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa maendeleo ya Tanzania katika suala la mtiririko wa misaada ya makubaliano baina ya nchi na nchi yaani ODA. Pia, Serikali ya Marekani ni mfadhili mkuu wa mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania. Katika sehemu inayofuata tunachunguza jinsi misaada ya makubaliano ya nchi na nchi na ile ya kimataifa, inayotoka Marekani inavyowasaidia watu wa Tanzania kufikia malengo ya maendeleo kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 kati ya 2012 hadi 2022.

Funzo #1. Serikali ya Marekani inaongoza kwa kutoa misaada ya maendeleo ya moja kwa moja ya makubaliano ya nchi na nchi inayochangia wastani wa dola za Kimarekani milioni 673 kila mwaka.

Kati ya mwaka 2012 hadi 2022, Serikali ya Marekani ilipeleka zaidi ya dola bilioni 7.4 (USD milioni 673 kila mwaka) kama msaada wa moja kwa moja wa makubaliano ya nchi na nchi kwa ajili ya kusaidia ukuaji na ustawi wa Tanzania, kiasi ambacho ni mara mbili ya mchangiaji mkuu aliyefuatia. Mwaka uliopita 2021, wa data inayolinganishwa nayo, kiwango cha msaada wa Serikali ya Marekani kilizidi kiasi cha washirika sita kwa pamoja (Tazama Jedwali Na. 2).[3] Wakala kumi na tisa wa serikali wa maendeleo ya Kimataifa walichangia juhudi hizo—kutoka kwa wadau wakuu wa maendeleo kama vile Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na MCC kwa michango iliyolenga sekta mahususi kutoka idara nyingine.[4]

Afya ya umma imekuwa lengo kuu la msaada wa makubaliano na Marekani (Jedwali Na. 3), hasa jitihad≥a za kupambana na VVU/UKIMWI (Dola za Kimarekani bilioni 3.8) na malaria (Dola za Marekani milioni 534). Kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, Marekani ilielekeza rasilimali zake kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania (Dola za Kimarekani milioni 546) na miundombinu muhimu (Dola za Kimarekani milioni 579). Idara za Ulinzi za Marekani ziliwezesha shughuli za kujenga uwezo na uhusiano na Tanzania (k.m., ushirikiano, elimu, na mafunzo) katika maeneo mbalimbali kama vile kupambana na dawa za kulevya na ujangili. Ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki, msaada wa kijeshi na kiusalama ulikuwa sehemu ndogo ya msaada wa makubalinao ya nchi na nchi wa Marekani kwa Tanzania, hali hii inatokana na hali ya usalama kuwa tulivu nchini Tanzania (BBC, 2023; START, 2022).

Jedwali Na. 2. Wafadhili wakuu wa misaada ya makubaliano ya nchi na nchi kwa Tanzania

Jina la mfadhili 2012-2022, Jumla ya milioni za USD 2021 USD zilizopokelewa
1 Marekani 7402.3 515.1
2 Jamhuri ya Watu wa China* (PRC) 3075.18 167.88
3 Uingereza (UK) 2520.05 90.27
4 Japani 1274.58 44.67
5 Uswidi 1184.42 89.34
6 Kanada 1076.30 52.33
7 Korea Kusini 783.12 63.30
8 Denimaki 771.46 54.61
9 Ujerumani 762.51 66.77
10 Norwei 748.33 55.26
Dokezo: Jedwali hili linaonyesha wafadhili 10 wakuu wa msaada wa makubaliano ya nchi na nchi kwa Tanzania (ikiwa ni pamoja na misaada, mikopo yenye masharti tofauti tofauti, na mikopo ya mauzo ya nje). Pesa za Jamhuri ya Watu wa China (PRC) zinawakilisha ahadi na sio malipo, kuanzia 2012-2021. Takwimu nyingine zote zinawakilisha malipo kati ya 2012 hadi 2022. Thamani zote ni za wastani wa Dola za Marekani kwa 2022. Chanzo: ForeignAssistance.gov (2012-2022), AidData’s Global Chinese Development Finance Dataset, Version 3.0.

Kielelezo 1. Msaada wa makubaliano ya nchi na nchi kutoka Serikali ya Marekani kwaTanzania, 2012-2022

Dokezo: Kielelzo hiki kinaonesha jumla ya msaada uliotolewa kwa makubaliano ya nchi na nchi kutoka Marekani (misaada, mikopo, usaidizi wa kiufundi, na mikopo ya mauzo ya nje) kwa Tanzania kila mwaka kuanzia 2012 hadi 2022. Takwimu hii inajumuisha msaada wa maendeleo na usalama unaotolewa moja kwa moja kupitia mashirika ya Serikali ya Marekani. Haijumuishi msaada unaotolewa na Marekani kupitia mashirika ya kimataifa ambayo pia yanaweza kuinufaisha Tanzania. Chanzo: ForeignAssistance.gov (2012-2022).

Jedwali Na. 3. Sekta 5 za juu zilizopata msaada wa Serikali ya Marekani kwa Tanzania, 2012-2022<

Jina la sekta ya Marekani Milioni za USD
zilizotolewa (wastani 2022)
Kiasi cha Mradi
VVU/UKIMWI 3778.85 6629
Miundombinu 579.07 370
Kilimo 546.10 1730
Malaria 533.53 1261
Gharama za Utawala 320.30 8205
Dokezo: Jedwali hili linaonyesha sekta tano za juu zilizopokea msaada wa serikali ya Marekani nchini Tanzania kuanzia 2012 hadi 2022. Chanzo: ForeignAssistance.gov (2012-2022).

Funzo #2. Serikali ya Marekani inatoa wastani wa dola za Marekani milioni 394 kila mwaka kusaidia juhudi za Tanzania kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza kama vile VVU/UKIMWI na malaria.

Serikali ya Marekani imekuwa mstari wa mbele kufanya kazi na serikali ya Tanzania na washirika wa sekta binafsi ili kukabiliana na changamoto kubwa za afya ya wananchi. Kama mfadhili mkubwa zaidi wa programu za kinga na matibabu ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania, Marekani ilitoa wastani wa dola milioni 345.1 kila mwaka tangu 2012. Shughuli hizo nyingi ziko chini ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) (Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Februari 2023), uliozinduliwa na aliyekuwa Rais wa Marekani, George W. Bush mwaka 2003. Miradi iliyofadhiliwa na PEPFAR ni pamoja na Mradi wa Kutunza Watoto na Kuwawezesha Vijana (C2EYP), ambao ulianza 2016 hadi 2021. Mpango wa C2EYP ulichukua mwelekeo wa kusaidia watoto yatima[5] wa Kitanzania na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, ujuzi wa ajira, na msaada wa kijamii kwa watoto na wazazi (USAID, 2016).

Mbali na VVU/UKIMWI, malaria ni mzigo mwingine mkubwa wa kiafya kwa kijamii na chanzo kikuu cha vifo vya watoto wa Kitanzania (PMI VectorLink, 2022). Katika kuitikia changamoto hiyo, Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya dola milioni 48.5 kwa mwaka, kwa wastani, kupitia Mpango wa Rais wa Marekani wa Malaria (PMI) ili kuwasaidia Watanzania kupunguza magonjwa na vifo vya watoto.

Miradi ya matibabu uzuiaji wa Malaria (John Snow Inc, 2016) kama vile PMI's VectorLink (2018-2023) lilikuwa ni jukumu muhimu: kuwalinda takribani Watanzania milioni 2 kwa mwaka kupitia upuliziaji salama wa dawa ya ndani ya muda mrefu (IRS), kusambaza vyandarua, na kutoa kinga binafsi, vifaa na kupuni za afya kwa watu binafsi (PMI, VectorLink, 2022). Kiungo cha Vekta ni sehemu tu ya zana inayofadhiliwa na USAID katika mapambano dhidi ya malaria, na inachangia chini ya asilimia 7.3 ya ufadhili wote ambao serikali ya Marekani imetoa kwa Tanzania.

Kielelezo 2. Msaada wa kila mwaka wa makubaliano ya nchi na nchi kutoka Serikali ya Marekani kwa ajili ya afua za VVU/UKIMWI nchini Tanzania, 2012-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha ufadhili wa kila mwaka wa serikali ya Marekani ambao ulielekezwa katika afua za VVU/UKIMWI nchini Tanzania kuanzia 2012 hadi 2022. Chanzo: ForeignAssistance.gov (2012-2022).

Kielelezo Na. 3. Msaada wa jumla wa wafadhili wote wa OECD kwa afua za VVU/UKIMWI nchini Tanzania, 2012-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha mchanganuo wa wafadhili wa OECD ambao walichangia katika afua za VVU/UKIMWI nchini Tanzania, kuanzia 2012 hadi 2022. Chanzo: OECD Creditor Reporting System (2012-2022).

Funzo #3. Kuongezeka kwa msaada wa Serikali ya Marekani katika kuisaidia Tanzania kunaifanya kuwa mhimili wa msaada wa chakula cha dharura kutoka kwa mpokeaji hadi kwa mwekezaji katika mifumo stahimilivu ya kilimo.

Kwa kuchangia theluthi moja ya Pato la Taifa la Tanzania na theluthi mbili ya kazi zake, kilimo ni msingi wa ustawi wa taifa (USAID, Agosti 2022). Mwanzoni mwa miaka ya 2000, karibu asilimia 100 ya misaada ya kilimo ya Marekani kwa Tanzania ilikuwa ni msaada wa dharura wa kundi la II. Hata hivyo, kati ya 2019 hadi 2022, chini ya asilimia 5 ya misaada ya Serikali ya Marekani kwa kilimo nchini Tanzania ilitumika kwa chakula cha muda mfupi. Badala yake, walio wengi walifadhili uwekezaji wa muda mrefu katika mifumo ya chakula ambayo ni thabiti ili kuimarisha minyororo ya thamani na mavuno katika maeneo ya uzalishaji wa nafaka (Kielelezo 4).

Mradi wa Feed the Future unaofadhiliwa na USAID (NAFAKA II) uliwafikia wakulima wapatao 300,000 na kuongeza kiasi cha mpunga na mahindi kilichouzwa na wazalishaji kwa asilimia 435 katika kipindi cha uhai wa mradi (ACDIVOCA, n.d.). Mabadiliko haya yanaakisi dira ya pamoja kwa Tanzania kuendeleza na kumiliki mfumo wa chakula ambao ni stahimilimilivu.

Hata hivyo, ingawa Marekani inaimarisha sekta ya kilimo kwa ujumla, haifumbii macho mahitaji ya haraka ya wananchi wa Tanzania na inawajibika kutekeleza vipaumbele vya muda mfupi. Ili kukabiliana na UVIKO-19 na kukatika kwa mifumo ya usambazaji wa chakula duniani mwaka 2020 na 2021, USAID ilikusanya zaidi ya dola milioni 20 kama misaada ya haraka ya kundi II, chini ya mwaka mmoja tangu kusimamisha mpango huo nchini Tanzania.

Kielelezo Na. 4. Msaada wa kila mwaka wa makubaliano ya nchi na nchi kutoka Serikali ya Marekani kwa sekta ya kilimo na Kundi la II la msaada wa dharura wa chakula nchini Tanzania, 2001-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha ufadhili wa kila mwaka wa serikali ya Marekani kwa sekta ya kilimo (mstari wa rangi ya bluu –nyeusi) na Kategoria II ya msaada wa dharura wa chakula (rangi ya machungwa) nchini Tanzania kuanzia 2001 hadi 2022. Chanzo: ForeignAssistance.gov (2012-2022).

Funzo #4. Uwekezaji endelevu wa miundombinu ya barabara, maji na nishati umekuwa wa muda mrefu, maeneo yaliyotiwa saini ya ushirikiano kati ya serikali ya Marekani na Tanzania.

Kwa kutambua kwamba miundombinu ni muhimu kwa ustawi wa kaya na uchumi mpana, Serikali za Marekani na Tanzania zilishirikiana kuwekeza rasilimali nyingi katika juhudi za kuimarisha miundombinu ya barabara, maji na nishati. Mkataba wa kwanza wa Tanzania (2008-2013) na MCC ulikuwa na Dola za Marekani milioni 698.1 kwa ajili ya ufadhili wa miundombinu, ikiwa ni pamoja na uwekezaji wa kuboresha barabara kuu tatu (Tanga-Horohoro, Tunduma-Sumbawanga, na Ushoroba wa Mtwara) na kujenga uwezo wa Wakala wa Barabara (TANROADS) katika kubuni na utekelezaji endelevu wa miradi mipya (MCC, Februari 2024). MCC ilisaidia pia upanuzi wa upatikanaji wa nishati, kukarabati vituo vya umeme vinavyohudumia wateja 215,000, kupanua njia 247 za usambazaji, na kujenga kebo ya umeme na mawasiliano ya simu ya chini ya bahari ya kilomita 40 inayounganisha Kisiwa cha Unguja na Bara.

Power Africa—mpango wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama wa kufadhili upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wote, na endelevu katika bara zima—ulizinduliwa nchini Tanzania Julai 2013 (AfDB, n.d.). Kwa kushirikiana na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), wakala wa Serikali ya Marekani, na makampuni ya sekta binafsi, Power Africa ilikusanya dola za Kimarekani milioni 2.7 kwa mwaka katika miradi ya kuzalisha nishati, kusambaza nishati, na kupanua uzalishaji wa umeme nchini kwa megawati 671. Taarifa za ziada kuhusu ushirikiano huu wa sekta ya umma na binafsi katika kuboresha upatikanaji na uhakika wa umeme wa Tanzania zimefafanuliwa katika sura inayofuata.

Funzo #5. Mafunzo na uimarishaji wa ujuzi umekuwa na msisitizo mkubwa katika msada wa Serikali ya Marekani kwa miaka ya hivi karibuni, hivyo kuisaidia Tanzania kuimarisha mtaji wake na ufanisi wa kazi.

Kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025 msisitizo wa kujenga uwezo wa nguvu kazi yenye tija, utendaji na ushindani (FYDP III), serikali ya Marekani ilitoa dola milioni 248.7 kwa ajili ya kusaidia mafunzo na kuendeleza ujuzi wa washirika wa Tanzania kati ya 2012 hadi 2022 (Kielelezo Na. 5). Mashirika na idara[6] kumi na tatu za Marekani, pamoja na mashirika sita ya kimataifa,[7] yalisaidia shughuli tofautitofauti 3,355 katika kipindi hicho.

Msaada wa kiufundi wa Marekani ulisaidia kujenga uwezo katika sekta mbalimbali. Ukuzaji wa nguvu kazi ilikuwa mada ya kawaida katika miradi mingi. Programu ya Mkapa Fellows (2020-2025) inalenga kuajiri wataalamu wa afya ili kupunguza uhaba wa wafanyakazi katika sekta ya afya (kwa sasa ni asilimia 56) (USAID, Januari 2023). Kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania, Benki ya Dunia (kwa msaada wa Serikali ya Marekani) imesaidia programu za mafunzo ya ufundi stadi au vyuo vikuu katika sekta muhimu za kiuchumi kwa wanafunzi wa Kitanzania 45,718 kupitia Mpango wake wa Elimu na Ujuzi kwa Ajira zenye Tija (ESPJ) (Benki ya Dunia, Juni 2023). Uimarishaji wa asasi za kiraia umekuwa lengo lingine muhimu, kama inavyoonekana katika Mradi wa Usimamizi wa Takwimu za USAID, ambao ulikusanya dola milioni 11.5 kusaidia mashirika 50 ya Kitanzania kuboresha ujuzi katika utetezi unaozingatia ushahidi, usimamizi wa shirika, na kuweka kumbukumbu za ukiukwaji wa haki za binadamu (USAID, Oktoba 2022).

Miradi mingine ya kujenga uwezo imelenga kuisaidia Tanzania kukuza uchumi wake kwa njia za kujihami dhidi ya vishawishi hasi. Kwa mfano, Kamandi ya Marekani barani Afrika, ilitumia zaidi ya dola milioni 8 kusaidia Serikali ya Tanzania katika mafunzo na vifaa vya kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya na uhalifu wa kupangwa chini ya Mpango wa Kimataifa wa Kupambana na Dawa za Kulevya (2009-2019) wa Idara ya Ulinzi ya Marekani (ForeignAssistance.gov; DOD, 2023). Mradi wa WEKEZA[8] (2012-2017) ulijikita katika kutoa huduma za kujikimu kwa kaya 5,383 na huduma za elimu kwa watoto 13,096 wanaojihusisha au waliopo katika hatari ya ajira za watoto (DOL, n.d.).

Kielelezo Na. 5. Msaada wa kila mwaka wa nchi na nchi na wa kimataifa kutoka Serikali ya Marekani kwa ajili ya kukuza ujuzi nchini Tanzania,2001-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha ufadhili wa kila mwaka wa serikali ya Marekani, kupitia makubaliano ya nchi na nchi na kimataifa, zinazoelekezwa katika kukuza ujuzi nchini Tanzania kuanzia 2001 hadi 2022. Chanzo: ForeignAssistance.gov (2012-2022) naOECD Creditor Reporting System (2012-2022). Makadirio yamekokotolewa na AidData.

Katika ulimwengu unaozidi kuunganishwa na kuwa kama kijiji unakabiliwa na vitisho changamani, ni muhimu kwa wanajeshi wawezeshwe kushirikiana na kuwasiliana miongoni mwao wenyewe. Marekani na Tanzania zimefanya mazoezi mengi ya pamoja ya kijeshi na shughuli za mafunzo katika muongo mmoja uliopita ili kuimarisha uhusiano wao kwa ajili ya utulivu na kuimarisha ushirikiano. Kati ya 2012 hadi 2019, karibu askari elfu tisa wa Tanzania walishiriki katika shughuli za mafunzo ya pamoja (Jedwali la 4). Maafisa kutoka Tanzania walijifunza ujuzi maalum katika kambi nyingi za kijeshi nchini Marekani, na maelfu ya wanajeshi walipata mafunzo kwa pamoja ili kusaidia shughuli za kikanda za kulinda amani.

Jedwali la 4. Idadi ya waliofundishwa katika mpango wa pamoja wa mafunzo ya kijeshi, 2012-2019

Mpango wa Marekani wa Mafunzo ya Kijeshi Idadi ya waliofundishwa (2012-2019)
Operesheni za Kulinda Amani 8461
Elimu na Mafunzo ya Kijeshi ya Kimataifa 179
Mpango wa Kupambana na Ugaidi 127

Idara ya Usalama wa Nchi - Shughuli za Ulinzi wa Pwani ya Marekani

99
Kituo cha Kikanda cha Mafunzo ya Kiusalama 90

Programu ya Kupambana na Ugaidi na Ushirika wa Vita Isiyopangwa

14
Ufadhili wa Kijeshi wa Kigeni 11
Akademia za huduma 3
Jumla ya waliofundishwa 8,984
Dokezo: Jedwali hili linaonyesha jumla ya idadi ya wanajeshi walioshiriki katika programu za mafunzo ya kijeshi ya kigeni kwa msaada wa Marekani. Jumla ya waliofundishwa katika programu huhesabiwa kulingana na programu, kila mwaka, na kwa hivyo wanaweza kuhesabiwa mara mbili watu ambao walishiriki katika shughuli nyingi. Hata hivyo, takwimu hii ni kiwakilishi cha jumla cha idadi ya fursa kwa Watanzania kupata mafunzo katika programu zote. Chanzo: Security Assistance Monitor (2012-2019).

Funzo #6. Takribani asilimia 25 ya misaada ya serikali ya Marekani kwa Tanzania inatolewa kwa ushirikiano na wafadhili wengine kwa ajili ya kusaidia miundombinu muhimu na miradi ya afya kwa wananchi.

Kwa juhudi za pamoja na washirika wengine wa maendeleo, Marekani ilitoa dola milioni 209 kila mwaka (kwa wastani) za msaada wa makubaliano ya nchi na nchi kati ya 2012 hadi 2022 kupitia taasisi za kimataifa (k.m., mashirika ya Umoja wa Mataifa, na benki za maendeleo za kikanda). Katika muongo uliopita, sehemu ya misaada ya USG kwa Tanzania iliyoelekezwa kupitia taasisi za kimataifa iliongezeka kutoka asilimia 18 mwaka 2012 hadi asilimia 39 mwaka 2022 (Kielelezo 7).

Uwekezaji katika miundombinu mikuu ya Tanzania ni sehemu muhimu ya tathmini hii. Inahusisha pamoja na msaada wa dola milioni 205 kutoka Benki ya Dunia ili kusaidia uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam Maritime Gateway (Benki ya Dunia, n.d.a) na Usafirishaji wa AFR RI-3A Tanzania-Zambia. Mradi wa miundombinu ya kuunganisha nishati (Benki ya Dunia, n.d.b), miongoni mwa mengine. Sehemu nyingine kubwa ya ufadhili huu ilitoka kwenye Mfuko wa Kimataifa (milioni 104) ili kukabiliana na VVU/UKIMWI na malaria.

Ingawa haijaelekezwa kwa Tanzania pekee, Marekani inatoa msaada muhimu katika mipango kadhaa ya kanda ya Afrika Mashariki. USAID ilisaini mkataba wa miaka mitano wa msaada wa dola milioni 28.7 mwaka 2016 ili kusaidia uratibu wa kikanda ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika maeneo manne: biashara na uwekezaji; kilimo; usimamizi wa mazingira na maliasili; na nishati (USAID, 2022a).

Mipango mingine ambayo ni vielelezo, ni pamoja na ushirikiano na Umoja wa Afrika kulinda viumbe hai vya baharini na kuzuia magonjwa ya mipakani yasiathiri mifugo ya Tanzania (USD 6.9 milioni) (IBAR n.d., IBAR 2015) na Mpango wa Uongozi kwa Vijana (YALI) na Kituo cha Uongozi cha Afrika Mashariki kusaidia maendeleo ya stadi kwa kizazi kijacho cha wafanyabiashara, mashirika ya kiraia, na wataalamu wa sekta ya umma katika nchi 14 ikiwa ni pamoja na Tanzania (USD milioni 22.4) (YALI, n.d.).

Kielelezo Na. 6. Sehemu ya msaada wa kila mwaka kutoka Serikali ya Marekani unaotolewa kupitia washirika wa kimataifa, 2001-2022

Dokezo: Takwimu hizi zinaonyesha makadirio ya jumla ya hisa (kushoto) na jumla ya thamani ya dola (kulia) ya michango ya Serikali ya Marekani kwa Tanzania ambayo ilitolewa kupitia taasisi za kimataifa kuanzia 2001 hadi 2022. Chanzo: ForeignAssistance.gov (2012-2022) and OECD Creditor Reporting System (2012-2022). Makadirio yalikokotolewa na AidData.

2.2 Mchango wa Serikali ya Marekani usio wa moja kwa moja kwa Tanzania

Katika sehemu iliyotangulia, tulieleza jinsi msaada wa moja kwa moja kutoka Serikali ya Marekani ulivyoisaidia Tanzania katika kuendeleza malengo ya maendeleo ya taifa. Hata hivyo, kuna jukumu la pili la Serikali ya Marekani ambalo lina nafasi ya kukusanya rasilimali nyingi za muda mrefu ili kuchochea ukuaji wa Tanzania: kukuza uwekezaji wenye tija, biashara na sera za uhamiaji ambazo zinainua uwezo wa sekta binafsi za Amerika. Ingawa michango hii ambayo si ya moja kwa moja ni vigumu kuiwasilisha kitakwimu, katika sehemu inayofuata tunaangazia mifano kadhaa, kama vile utumiaji wa dhamana ya bima, makubaliano ya biashara ya masharti nafuu, na viza kwa wanafunzi, wasomi na wataalamu wabobezi.

Funzo #7. Msaada wa kifedha unaotolewa na Serikali ya Marekani na dhamana ya bima imeisaidia Tanzania kuvutia takribani dola milioni 93.3 za uwekezaji katika sekta binafsi tangu mwaka 2012.

Mpango wa Dira ya 2025 wa Tanzania unabainisha uwekezaji wa nje wa moja kwa moja (FDI) kama chanzo kikuu cha sekta binafsi ya nje kufadhili ajenda yake. Udhamini wa fedha na bima[9] unaodhaminiwa na Serikali ya Marekani una jukumu muhimu katika kuongeza imani ya wawekezaji wa kigeni wanaotarajia kupunguziwa vihatarishi vya kisiasa na ukosefu wa uelewa wa soko la ndani kwa ajili ya kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.

Shirika la Fedha la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (DFC), ambalo awali lilijulikana kama Shirika la Uwekezaji Binafsi Ughaibuni (OPIC), ni wakala huru wa serikali anayesaidia mashirika ya Kimarekani kufanya biashara na kuwekeza katika nchi za kipato cha chini na cha kati. Kati ya 2012 hadi 2022, Serikali ya Marekani ilitoa dola milioni 79.2 (takribani dola milioni 7.2 kwa mwaka) kwa ajili ya ufadhili wa bima ya vihatarishi kwa miradi 8 ya kupanua uchukuzi, biashara ndogondogo na za kati (SMEs), na upatikanaji wa nyumba nchini Tanzania. Mradi mkubwa zaidi kati ya hiyo ulikuwa dhamana ya bima ya dola milioni 31.3[10] mwaka 2017 kwa ajili ya kusaidia Kampuni ya Alistair James Limited kupanua usafirishaji katika shughuli zake nchini Tanzania. DFC pia ilisaidia miradi mitatu mwaka 2022 ambayo ilipanua bima na mikopo kwa SMEs na wanunuzi wa nyumba ambao ni wanawake (DFC, n.d.a; DFC, n.d.b).

Vile vile, Marekani inasaidia shughuli za Wakala wa Dhamana ya Uwekezaji wa Kimataifa wa Benki ya Dunia (MIGA) ili kutoa dhamana ya uwekezaji katika sekta ya biashara ya kilimo, madini, mawasiliano, utengenezaji na huduma za kifedha. Mwaka 2014 na 2015, MIGA ilisaidia shughuli mbili za bima ya vihatarishi vya kisiasa kwa kampuni ya Silverlands Tanzania Limited, ambayo ni mfanyabiashara wa kuku, huku michango ya Marekani ikikadiriwa kuwa dola milioni 14.1 na kusaidia ajira 925 (MIGA, n.d.). Kwa pamoja, msaada wa Marekani kwa ajili ya dhamana ya uwekezaji kupitia DFC na MIGA umeiwezesha Tanzania kuvutia wastani wa dola za Marekani milioni 93.3 katika uwekezaji wa sekta binafsi tangu mwaka 2012 (Kielelezo Na. 7). Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, uwiano umebadilika wakati MIGA ikipunguza hadi kutia saini mikataba miwili tu na Tanzania, DFC imeimarisha shughuli zake na sekta binafsi nchini Tanzania.

Kielelezo Na. 7. Jumla ya msaada wa uwekezaji unaotolewa na Serikali ya Marekani kupitia MIGA na DFC, 2000-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha makadirio ya jumla ya msaada wa uwekezaji uliotolewa na Serikali ya Marekani kupitia MIGA na DFC nchini Tanzania kuanzia 2000 hadi 2022. Chanzo: Shirika la Fedha za Maendeleo (2012-2022), Wakala wa Dhamana ya Uwekezaji wa Kimataifa wa Benki ya Dunia (2012-2022). Makadirio yamekokotolewa na AidData.

Funzo #8. Mauzo ya Tanzania kwenda Marekani yaliongezeka kwa asilimia 16 tangu 2016, na kunufaika na sera za kibiashara za masharti nafuu.

Kukuza wigo wa mauzo ya nje ya Tanzania ni muhimu kwa ajili ya ushindani wa kiuchumi. Juhudi kama vile Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika (AGOA), iliyopitishwa mwaka 2000, imefungua ufikiwaji wa soko la Marekani bila ushuru kwa zaidi ya bidhaa 1,800.[11] Kifungu maalumu katika sheria hiyo kinaitaka Marekani kuagiza nguo kutoka nchi zenye mkataba wa AGOA kama ilivyo Tanzania kabla ya kutafuta kutoka nchi zingine. Mnamo mwaka 2013, Serikali ya Marekani ilizindua na kusaini mpango wa pili wa biashara: Kitovu cha Biashara na Uwekezaji cha Afrika Mashariki chini ya mpango wa Biashara Afrika. Kitovu hicho kilivutia dola za Kimarekani milioni 74 kati ya 2014 na 2021 ili kuwezesha utangamano, biashara, na uwekezaji katika Afrika Mashariki (USAID, n.d.). Matokeo yanatia moyo, kwani kituo hicho kinakadiriwa kuwezesha zaidi ya wanunuzi wa mauzo ya nje 800 na kutengeneza ajira mpya 33,000 zinazowanufaisha watu wa Tanzania na majirani zao wa Afrika Mashariki (USAID, 2017).

Mipango hii ya kisera imezaa matunda, na kuimarisha biashara kati ya Marekani na Tanzania. Tangu mwaka 2012, uagizaji wa bidhaa wa Marekani kutoka Tanzania umeongezeka kwa asilimia 16—kutoka dola milioni 146 hadi dola milioni 170. Ingawa ukuaji huu ulipungua kidogo wakati wa janga la UVIKO-19, uliongezeka kwa kiasi kikubwa mwaka 2022 (+Dola milioni 61.4), ukionesha manufaa thabiti ya sera za biashara na kuendelea na dhamira ya dhati ya waagizaji wa Marekani katika ukuaji wa pamoja na wauzaji wa bidhaa za nje kutoka Tanzania.

Kielelezo Na. 8. Jumla ya thamani ya uagizaji wa Marekani kutoka Tanzania, 2000-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha jumla ya thamani ya uagizaji wa Marekani kutoka Tanzania, kuanzia 2000 hadi 2022. Chanzo: World Bank Group World Integrated Trade Solution (2000-2022).

Funzo #9. Takribani wanafunzi na wasomi 1,100 wa Kitanzania hunufaika kwa kusoma katika taasisi za elimu ya juu za Marekani kila mwaka ili kuendeleza taaluma zao

Kwa lengo la kuufanya uchumi kuwa wa kisasa, Tanzania inahitaji nguvukazi yake ya ndani iwe na ujuzi wa kisasa ili kuongeza ukuaji wa viwanda na kuboresha tija ya sekta ndogondogo za kilimo. Katika kuunga mkono lengo hili, Serikali ya Marekani hutoa fursa kwa wanafunzi na wasomi wa Kitanzania katika mafunzo na elimu kwenye taasisi za elimu ya juu za Marekani kupitia programu za hati za kusafiria na viza zilizoundwa kwa ajili ya wanafunzi (viza F-1) na wasomi (visa J-1). Programu hizi zimewezesha wastani wa wanafunzi na wasomi wa Kitanzania 1,095 kusoma nchini Marekani kila mwaka kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita.[12]

Licha ya kuwapa Watanzania fursa ya kupata ujuzi wa soko unaohitajika kwa kazi zenye malipo makubwa, taasisi za Marekani pia zinakuza maendeleo ya kizazi kijacho cha viongozi wa Tanzania, ili kuwa na fikra za kimataifa, na wavumbuzi. Viongozi na wasomi wengi wa Tanzania wamehitimu shahada kutoka vyuo vikuu vilivyoko Marekani. Mfano mmoja mashuhuri ni Dkt. Mohamed Bilal aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, ambaye alipata shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Howard na Ph.D. katika fizikia kutoka Chuo Kikuu cha California, Berkeley.

Wanafunzi na wasomi wa Kitanzania hupokea kiasi cha dola milioni 3.7 kila mwaka kama msaada wa kifedha wakati wa masomo yao kupitia ufadhili wa masomo unaotolewa na vyuo vikuu vya Marekani au programu za Serikali ya Marekani (Kielelezo Na. 9), kama vile Ufadhili wa Fulbright au Mpango wa Uongozi wa Wageni wa Kimataifa. Fursa nyingine kwa wanafunzi wa Kitanzania na wasomi kuweza kunufaika na mafunzo nchini Marekani ni pamoja na Mpango wa Viongozi Vijana wa Afrika ujulikanao kama Mandela Washington Fellowship, Mpango wa Uongozi wa Vijana wa Umajumui wa Afrika (PAYLP) na Programu ya Kennedy-Lugar Youth Exchange and Study (YES).

Makadirio haya yanatokana na wastani wa takribani nafasi 100 za ufadhili wa masomo na programu za mabadilishano zinazotolewa kwa wanafunzi wa Kitanzania kwenda kusoma Marekani kila mwaka, na marupurupu yanayotolewa kwa wanafunzi wanaosoma programu za uzamivu (Ph.D) katika taasisi za Marekani kwa mwaka wowote kati ya 2014 na 2023. Haya ni makadirio ya chini na yanaweza kushindwa kuonesha uhalisia wa manufaa kamili ya kifedha kutoka Marekani kwa wanafunzi wa Kitanzania.

Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma shahada za uzamivu nchini Marekani kwa ujumla hufadhiliwa kwa asilimia mia moja na taasisi zinazowadahili, ikiwa ni pamoja na ada ya masomo, bima ya afya, na malipo ya kujikimu. Haya ni makadirio ya chini na kuna uwezekano kuwa hayaoneshi thamani halisi ya msaada wa elimu wa Marekani kwa wanafunzi na wasomi wa Kitanzania. Baadhi ya watu wanaosoma viwango vingine vya elimu (k.m., shahada ya kwanza, shahada ya umahiri, na ngazi ya cheti) wanaweza pia kupata msaada wa kifedha kutoka kwenye taasisi wanazowadahili au Serikali ya Marekani.

Kielelezo Na. 9. Makadirio ya dolla za udhamini na kujikimu zinazotolewa kwa wanafunzi wa Kitanzania nchini Marekani,2014-2023

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha makadirio ya thamani ya kila mwaka ya ufadhili wa masomo na marupurupu yanayotolewa kwa wanafunzi wa Kitanzania nchini Marekani kuanzia 2014 hadi 2023. Chanzo: Idara ya Serikali ya Marekani na Idara ya Usalama wa Taifa ya Mfumo wa Taarifa za Wanafunzi na Ubadilishanaji wa Wageni (SEVIS) (2014-2023). Makadirio yamekokotolewa na AidData.

Wakati wanafunzi na wasomi wengi wanarudi Tanzania baada ya kuhitimu masomo yao, baadhi yao hujiunga na wafanyakazi wa Marekani katika kwa kazi maalumu kupitia mpango wa viza wa H-1B. Mpango huu unaruhusu wafanyakazi wenye ujuzi wa juu kutoka nchi za kigeni kuwa sehemu ya wafanyakazi wa Marekani na kupata ujuzi na uzoefu muhimu kazini. Njia nyingine inayotoa fursa kwa raia wa Tanzania kufanya kazi nchini Marekani ni kupitia ukazi wa kudumu.

Kwa mujibu wa takwimu za Idara ya Usalama wa Taifa ya Marekani, kati ya 2013-2022, wastani wa raia 1,634 wa Tanzania walipata hati ya ukaazi wa kudumu nchini Marekani. Raia wa Tanzania wanaofanya kazi Marekani, kupitia fursa tofauti za viza, wakati mwingine hutuma fedha katika nchi yao ambayo huleta manufaa, kama inavyofafanuliwa katika Sura ya 3.

Katika sura hii, tuliangazia njia kadhaa ambazo serikali ya Marekani inatumia kutoa misaada, mikopo, na msaada wa kiufundi kupitia makubaliano ya nchi na nchi na za kimataifa ili kusaidia watu wa Tanzania katika kukuza maendeleo ya nchi yao kulingana na Dira ya Tanzania ya 2025. Pia, tulichambua jinsi serikali ya Marekani ilivyokuwa na jukumu la kukuza sera nzuri za ndani za Marekani zinazohusiana na uwekezaji, biashara, na uhamiaji na uwezekano wa kuruhusu ushiriki mkubwa wa sekta binafsi wa makampuni ya Marekani na taasisi za elimu ya juu katika kutengeneza ajira, kuongeza upatikanaji wa mtaji, na ujuzi wa wafanyakazi wa ndani. Katika sura inayofuata, tunachunguza jinsi raia wa Marekani na Tanzania wanavyojenga mahusiano yenye manufaa kwa pande zote mbili, ukiondoa nafasi ya Serikali ya Marekani.

Sura 3: Makampuni, mashirika na watu binafsi wa Marekani wanachangiaje ustawi wa Tanzania?

Ushirikiano wa Marekani na Tanzania unavuka mipaka ya uhusiano baina ya serikali na serikali. Mara nyingi huwa ni vigumu kutathmini nguvu ya makampuni ya Marekani, wahisani, vyuo vikuu, mashirika ya kiraia na watu binafsi wanaofanya kazi pamoja na wenzao wa Tanzania ili kufikia malengo ya pamoja. Katika sura hii, tunajaribu kuziba pengo hilo la ufahamu kwa kuchunguza mwelekeo tofauti wa ushirikiano huu wa jamii nzima kati ya Tanzania na Marekani—kutoka uhisani binafsi na msaada wa mtu na mtu hadi mwingiliano wa soko la utalii na uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja.

Kwa jumla, tunakadiria kwamba makampuni, mashirika na watu binafsi wa Marekani huchangia takriban dola bilioni 1.8[13] kila mwaka kwenye uchumi wa Tanzania. Michango hii ya wastani ya kila mwaka ni pamoja na dola milioni 96.3 za ufadhili wa watu binafsi, dola bilioni 1.3 za uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja, dola milioni 317.7 katika mtiririko unaohusiana na utalii, na dola milioni 103.7 kutoka kwa Watanzania wanaofanya kazi Marekani. Katika sehemu ya sura hii pia tunachambua kila moja ya njia hizo nne ili kuelewa jinsi zinavyoleta thamani kwa Watanzania.

3.1 Uhisani binafsi wa Marekani kwa raia wa Tanzania

Licha ya njia za kawaida za uhusiano kati ya serikali kwa serikali, taasisi za uhisani za Marekani zinachangia ukuaji na maendeleo ya Tanzania kwa njia mbalimbali kama vile kufadhili miradi ya msingi na kutoa msaada muhimu kwa mashirika ya ndani na kimataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania. Sambamba na hilo, uboreshaji wa teknolojia ya habari, mawasiliano, na usafirishaji umeongeza urahisi wa Wamarekani binafsi kushirikiana na wenzao wa Tanzania kupitia utalii na uhisani. Katika sehemu hii, tunachunguza jinsi taasisi za uhisani binafsi za Marekani na msaada wa watu kwa watu zinavyosaidia Tanzania kufikia malengo yake ya ukuaji na maendeleo kulingana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025.

Funzo #10. Taasisi 22 binafsi za Marekani na mashirika ya hisani yalikusanya dola milioni 96.3 kila mwaka kusaidia maendeleo ya Tanzania kuelekea Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025.

Baadhi ya wafadhili wakubwa wa Sekta binafsi duniani ni wahisani wa Marekani wanaohusishwa na makampuni ya Marekani: Shirika la Arcus, Shirika la Bill & Melinda Gates, Shirika la Conrad N. Hilton, Shirika la David & Lucile Packard, Shirika la Ford, na Shirika la John D. & Catherine T. MacArthur, miongoni mwa wengine. Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ndilo eneo kubwa zaidi la kijiografia linalovutia takriban theluthi moja ya uwekezaji wa maendeleo (Burgess na Custer, 2023). Nchini Tanzania, taasisi 22 za wahisani zenye makao yake nchini Marekani zilikusanya takribani dola milioni 96.3[14] kila mwaka kati ya 2012 hadi 2022 ili kufadhili shughuli za maendeleo.[15] Hii ni pamoja na ufadhili unaotolewa baina ya mashirika ya hisani pamoja na ufadhili unaotolewa kupitia vyombo vyaafya kimataifa, kama vile Muungano wa GAVI, Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Zaidi ya wahisani wa makampuni, majukwaa ya ufadhili wa watu mtandaoni yanafungua fursa mpya kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kupata mitaji kwa njia ya mikopo midogo midogo ili kuanzisha au kuongeza biashara ndogondogo au kusaidia familia zao. Badala ya msaada wa taasisi hadi taasisi, majukwaa haya ya ufadhili wa watu wengi yanaruhusu Waamerika binafsi kushirikiana moja kwa moja na wenzao wa Tanzania, kutoa mikopo midogomidogo kuanzia chini ya dola 25 na kuendelea. Shughuli hizi ndogondogo za watu kwa watu sio tu muhimu kwa wajasiriamali binafsi bali pia zinaongeza rasilimali kubwa nchini. Jukwaa moja tu la mikopo midogomidogo, mfano Kiva, liliwezesha mikopo midogomidogo yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 3.6 kutoka kwa watu wa Marekani kwenda kwa watu binafsi na biashara zao nchini Tanzania kati ya 2012 na 2022. Ingawa takwimu hii haileti ulimwengu wa uhusiano kati ya watu na watu, inatumika kama kielelezo cha ushirikiano thabiti kati ya nchi hizo mbili na uchumi wao.

Kielelezo Na. 10. Michango kutoka taasisi za uhisani za Marekani kwa Tanzania, 2012-2022

Dokezo: Jedwali hili linaonyesha jumla ya michango iliyotolewa na taasisi za uhisani za Marekani kwa Tanzania kila mwaka kuanzia 2012 hadi 2022. Takwimu hii inajumuisha mashirika 22 ya misaada ya kibinafsi pamoja na ufadhili wa Shirika la Bill & Melinda Gates kupitia taasisi za kimataifa. Chanzo: kanzidata ya Mfumo wa Kuripoti Wadai wa OECD (CRS).

3.2 Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja unaokuza mafanikio ya pamoja nchini Tanzania

Ufadhili wa hisani na msaada unaoelekezwa na serikali ni muhimu kwa maendeleo lakini bila shaka ni mdogo zaidi kimawanda na si endelevu kuliko aina nyingine za ushirikiano wa kiuchumi (Burgess na Custer, 2023). Kupunguza vikwazo kwa uwekezaji wa sekta binafsi kwa kiwango kikubwa ni kipaumbele muhimu kwa viongozi wa Tanzania, huku Rais Samia Suluhu Hassan akiweka mwelekeo wake wa kufikia dola bilioni 15 katika mtiririko wa kila mwaka wa FDI ifikapo mwaka 2025 (Christopher, 2023). Tanzania tayari ni miongoni mwa nchi 10 zinazoongoza kwa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja barani Afrika na ni soko la kuvutia kwa mitaji ya sekta binafsi yenye uwezo wa rasilimali hizo ili kuchochea ajenda yake ya maendeleo (Okafor, 2023; UNCTAD, 2023). Marekani, kama mshirika mkubwa zaidi wa FDI duniani kote kwa mwaka 2022 (BEA, 2023), ina historia ndefu ya kuwekeza nchini Tanzania na kuna nafasi ya kutosha ya kukuza ushirikiano huo wa sekta binafsi kwa siku za usoni.

Funzo #11. Makampuni ya Marekani yanaiona Tanzania kama kivutio cha uwekezaji kinachohitajika: wanatumia bilioni 1.3 kila mwaka katika hisa za FDI na kusaidia kutengeneza nafasi za ajira katika sekta ya nishati na utalii.

Tangu mwaka 2010, makampuni ya Marekani yamewekeza takribani dola bilioni 14.36 nchini Tanzania. Ingawa viwango vya FDI[16] vinatofautiana mwaka hadi mwaka (Kielelezo Na. 11), makampuni ya Marekani yana wastani wa dola za Marekani bilioni 1.3 kila mwaka katika hisa za FDI kwenye uchumi wa Tanzania kuanzia mwaka 2012 na kuendelea (Financial Times, n.d.). Sekta zinazohusiana na nishati kama vile makaa ya mawe, mafuta na gesi, na nishati mbadala zilivutia kiasi kikubwa zaidi cha mtaji wa uwekezaji wa Marekani kati ya mwaka 2010 na 2022, ikichukua jumla ya dola milioni 851.3 (Tazama Jedwali Na. 3 katika Sura ya 2).

Akiba ya kutosha ya gesi asilia nchini Tanzania katika pwani ya kusini imevutia mashirika mengi ya kimataifa kuwekeza nchini, huku Marekani ikiwa mhusika mkuu. Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi ya Marekani ya Symbion Power ilipata mtambo wa kuzalisha umeme wa MW 120 wa gesi asilia Ubungo, Dar es Salaam mwaka 2011 na pia ilijenga mitambo miwili ya dharura Dodoma (MW 55) na Arusha (MW 50) ili kusambaza umeme kwenye gridi ya taifa ya Tanzania wakati wa ukame, uhaba wa maji unapodhoofisha rasilimali za umeme wa maji. Mnamo mwaka 2013, Rais wa Marekani wa wakati huo Barack Obama alizindua Mpango wa Nishati wa Serikali ya Marekani kwa Africa katika Mtambo wa kuzalisha umeme wa Symbion.

Licha ya kuleta mitaji, FDI inaweza pia kutengeneza nafasi za kazi ambazo zitanufaisha wafanyakazi wa Tanzania. Sekta ya hoteli na utalii, ambazo ni mwajiri namba tatu kwa ukubwa nchini Tanzania, inaongoza kwa nafasi za kazi zilizotengenezwa kutokana na uwekezaji wa nje wa moja kwa moja wa Marekani (U.S. FDI) (Financial Times, n.d.). Sekta za madini, vyakula na vinywaji, mafuta, makaa ya mawe, na gesi pia zinaongoza katika kutengeneza nafasi za ajira kupitia U.S. FDI (ibid).

Sekta za huduma kama vile fedha, biashara, programu za TEHAMA pia zinavutia sehemu kubwa ya FDI kutoka Marekani na zinaonesha matumaini ya kukua kwa mtaji na kazi zenye hadhi ya juu (keshatajwa). Kwa mujibu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (2015), Marekani kupitia FDI ilisaidia kutengeneza jumla ya ajira 55,746 nchini Tanzania kati ya mwaka1990 na 2015.

Kielelezo Na. 11. Jumla ya dola za uwekezaji wa FDI wa Marekani nchini Tanzania, 2012-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha hisa ya kila mwaka ya uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja wa Marekani (FDI) nchini Tanzania kuanzia mwaka 2012 hadi 2022. Dola za FDI ni milioni za dola za Kimarekani. Chanzo: Ofisi ya Uchambuzi wa Kiuchumi ya Marekani.

Jedwali la 5. Sekta 10 za juu zinazovutia uwekezaji wa makampuni ya Marekani nchini Tanzania, 2010-2023

Nafasi Sekta Jumla ya FDI
(millioni za USD)
1 Makaa, Mafuta& gesi 670.6
2 Nishati jadidifu 180.7
3 Mawasiliano 119.5
4 Hoteli & Utalii 100.3
5 Huduma za Biashara 83.4
6 Huduma za Fedha 45.9
7 Programu & Huduma za TEHAMA 26.6
8 Madini 24.5
9 Chakula & Vinywaji 23.7
10 Usafirishaji & Maghala 14.8
Dokezo: Jedwali hili linachanganua dola za uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni katika sekta 10 kubwa zaidi ambazo makampuni ya Marekani yalishiriki katika kuwekeza nchini Tanzania, zikiorodheshwa kwa kiwango cha thamani. Dola za FDI ziko katika mamilioni ya dola. Chanzo: kanzidata ya Masoko ya Financial Times fDi.

3.3 Dola za Utalii na Utumaji wa Fedha kutoka Marekani zinazonufaisha uchumi wa Tanzania

Tanzania hupokea mamia ya maelfu ya wageni wa kimataifa kila mwaka, wakivutiwa na hifadhi ya Serengeti, Mlima Kilimanjaro, na fukwe za Zanzibar, miongoni mwa vivutio vingine vya utalii. Marekani ni miongoni mwa masoko matano (5) ya juu ya utalii nchini Tanzania, ikichukua asilimia 11 ya watalii wa kimataifa (Ofisi ya Taifa ya Takwimu, 2022) na chanzo kikubwa cha mapato.[17] Zaidi ya hayo, kama ilivyojadiliwa katika Sura ya 2, Marekani inawatambua Watanzania wengi wanaoishi ng'ambo, ama kwa muda mfupi au kwa kudumu, ambao hutuma baadhi ya mapato yao nyumbani kwa njia ya miamala (k.m., uhamishaji wa fedha kutoka kwa mfanyakazi wa kigeni kwenda kwa mtu binafsi nyumbani). Katika sehemu hii, tunaangalia kwa undani jinsi utalii wa Marekani na fedha zinazotumwa kutoka nje zinavyozalisha mapato yanayoweza kunufaisha kaya binafsi na uchumi wa Tanzania kwa ujumla wake.

Funzo #12. Marekani ni chanzo kikuu cha soko la utalii na mtiririko wa fedha zinazotumwa Tanzania hivyo kutoa mchango mkubwa wa fedha za kigeni na Pato la Taifa.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania, idadi ya watalii wa Marekani ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya watalii kutoka nchi nyingine. Kwa wastani, wanatumia Dola 400-495/mtu/siku—mara mbili ya mtu anayetumia pesa nyingi zaidi.[18] Dola hizo zote zinahesabiwa katika sekta ya utalii, ambayo ni chanzo kikubwa zaidi cha fedha za kigeni nchini Tanzania, mchangiaji namba mbili wa Pato la Taifa, na mwajiri namba tatu kwa ukubwa nchini (World Bank Group, 2021).

Mapato ya utalii kutoka Marekani hadi Tanzania yaliongezeka kwa kasi kwa muda wa miongo miwili iliyopita (Kielelezo Na. 12), na kuleta wastani wa dola za Kimarekani milioni 317.7 kwa mwaka kati ya 2012 hadi 2022. Janga la UVIKO-19 na vikwazo vingine vya usafiri vilitatiza mtiririko huo kwa muda; hata hivyo, kulikuwa na ufufuo wa haraka wa viwango vya kabla ya janga mwaka 2022. Juhudi za serikali ya Tanzania kukuza sekta yake ya utalii na nchi ya Marekani- kwa mfano hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhudhuria maonyesho ya kimataifa ya filamu ya utalii "Tanzania: The Royal Tour ” huko New York (Travel Agent Central, 2022)—na safari za ndege za moja kwa moja zilizopangwa kati ya nchi hizo mbili kuanzia mwaka 2024 (The Citizen, 2023) huenda zikaongeza idadi ya watalii Wamarekani nchini Tanzania na kuleta mapato zaidi.

Kielelezo Na. 12. Watalii wa Marekani na mapato yanayohusiana nayo kwa Tanzania, 2000-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha makadirio ya mapato kutoka kwa watalii wa Marekani wanaotembelea Tanzania kila mwaka kati ya 2000 na 2022. Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Tanzania.

Zaidi ya utalii, Marekani ndiyo inayoshika nafasi ya juu (Statista, n.d.) kwa kutuma fedha nchini Tanzania. Pesa hizo ni msaada muhimu wa kifedha kwa wanafamilia kuwawezesha kukabiliana na hali mbaya ya hewa au kuongeza mapato yao. Pia, zinaweza kutoa mtaji ili kuchochea shughuli za ujasiriamali binafsi au kuwekeza katika biashara za Tanzania au mali isiyohamishika. Kati ya mwaka 2012 na 2022, watu binafsi, familia na makampuni ya Kitanzania yalipata wastani wa dola za Kimarekani milioni 103.7 kila mwaka kutoka kwa watumaji nchini Marekani. Uhamishaji huo wa fedha kutoka Marekani hadi Tanzania umeongezeka kwa kasi katika muongo mmoja uliopita (Kielelezo Na. 13), licha ya majanga ya kimataifa kama vile UVIKO-19 na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kielelezo Na. 13. Makadirio ya pesa zinazotumwa kutoka Marekani kwenda Tanzania, 2012-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha makadirio ya fedha zinazotumwa kutoka kwa Watanzania wanaoishi Marekani kati ya mwaka 2012 na 2022. Chanzo: The World Bank’s Bilateral Remittance Matrix. Makadirio yamekokotolewa na AidData.

Katika sura hii, tumeelezea njia kadhaa ambazo makampuni ya sekta binafsi ya Marekani, mashirika ya hisani, na watu binafsi wanazozitumia kujenga uhusiano na wenzao wa Tanzania kwa njia zinazonufaisha ukuaji na maendeleo ya Tanzania. Tulichunguza jinsi mahusiano hayo kati ya watu na watu yanavyosaidia ushirikiano kati ya serikali na serikali, na hivyo kuruhusu Tanzania kutumia vyanzo mbalimbali vya mapato na kuingia katika mitaji ya ziada na utaalamu ili kuchochea uchumi wake. Katika sura inayofuata, tunachunguza njia ambazo ushirikiano huu unaweza kuchangia katika kuleta manufaa ya kiuchumi, kijamii na kiutawala kwa Tanzania, pamoja na jinsi uhusiano wa Tanzania na Marekani unavyotazamwa na viongozi wa Tanzania.

Sura 4: Kuna faida gani za wazi na zinazotarajiwa katika ushirikiano wa Marekani na Tanzania?

Awali, tulibainisha michango ya Marekani katika ukuaji na mafanikio ya Tanzania kwa njia mbalimbali, kupitia milioni za dola zinazokusanywa kila mwaka kwa wastani kupitia idadi ya vyanzo vya serikali, vyanzo binafsi, na njia za mtu mmoja mmoja. Hata hivyo, ushirikiano wa kudumu ni zaidi ya ufadhili, kwani nchi zote mbili zina nia ya pamoja ya kuona Tanzania inafikia malengo ambayo imejiwekea katika Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025.

Katika sura hii, tunapitia maendeleo ya Tanzania katika maeneo manne muhimu ya ushirikiano na Marekani (nishati, biashara, afya na elimu) ili kufuatilia jinsi ushirikiano na Marekani unavyoweza kuchangia kwa vitendo katika kuboresha ustawi wa Tanzania (Sehemu ya 4.1). Pia, tuliwadodosa na kuwasaili kwa kina viongozi wa Tanzania wanaofanya kazi katika sekta 13 ili kupima jinsi walivyouchukulia ushirikiano wa Marekani na Tanzania. Tuliwaomba viongozi wa umma, wa sekta binafsi na mashirika ya kiraia kutoa maoni yao kuhusu kiwango cha shughuli za Marekani wanazoziona katika sekta zao kuwa zina mchango muhimu kiasi gani katika maendeleo ya Tanzania; na masuala mengine yanayohusiana nayo (Sehemu ya 4.2).

4.1 Ushirikiano wa Marekani na Tanzania unawanufaishaje watu katika maisha yao ya kila siku?

Ili kujibu swali hili, tunachunguza mifano minne tofauti kutoka sekta ambazo Marekani imewekeza kwa sehemu kubwa ya misaada yake ya kifedha na kiufundi kwa Tanzania katika miongo miwili iliyopita. Kwanza, tulitathmini jinsi ushirikiano na Marekani unavyoweza kuchangia juhudi za Tanzania kupanua uwezo wake wa kuzalisha umeme na kupanua upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa watu wengi zaidi. Pili, tulipitia jinsi Tanzania inavyotumia sera za kibiashara za masharti nafuu kama vile Sheria ya Fursa ya Ukuaji wa Afrika ili kuingiza bidhaa bila ushuru kwenye soko la Marekani kwa mauzo yake ya nje.

Tatu, tulichunguza jinsi uwekezaji unaofanywa na Tanzania na Marekani katika kuimarisha uwekezaji kwenye afya ya wananchi na kukabiliana na magonjwa mahususi unavyoweza kuchangia kuongeza umri wa kuishi kwa tija. Hatimaye, tulichunguza jinsi uwekezaji katika kusoma, kuandika na kuhesabu kunavyoweza kuboresha viwango vya elimu na usawa wa kijinsia.

Funzo #13. Kwa kushirikiana na watu wa Tanzania, Marekani ilichangia ongezeko mara nne ya uzalishaji wa umeme na kusaidia kuendeleza sekta ya gesi asilia.

Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, uwekezaji endelevu kutoka Marekani, kwa Serikali ya Tanzania, na washirika wengine katika gridi ya umeme ya Tanzania (kama ilivyoelezwa katika Sura ya 2 na 3) umesaidia kuwa na umeme wa kuaminika zaidi na na hivyo kuwafikia watu wengi zaidi. Tangu mwaka 2000, upatikanaji wa umeme umeongezeka zaidi ya mara nne, na kuwafikia karibu asilimia 45 ya Watanzania mwaka 2021 (Kielelezo Na.14). Sehemu moja ya maelezo ya mafanikio haya ni mseto wa vyanzo vya nishati hiyo nchini Tanzania (Kielelezo Na. 15), kutoka kwenye kutegemea nishati ya maji hadi uwezo unaokua wa kuzalisha umeme kutokana na gesi asilia (na nishati jadidifu, kwa kiwango kidogo) (USITA, 2022).[19] Jumla ya uwezo wa umeme wa Tanzania katika vyanzo vyote vya nishati ulifikia MW 1,938 mwishoni mwa mwaka 2023 na serikali inalenga kuongeza zaidi hadi MW 5,000 ifikapo mwaka 2025, kutokana na kuongezeka kwa matumizi yake ya gesi asilia (TanzaniaInvest, 2023).

Mpango wa Power Africa- ambao ni ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi kati ya makampuni 170 ya Marekani na mashirika 12 ya serikali ya Marekani-imekuwa hatua muhimu ya ushiriki wa Marekani katika kusaidia mseto na upanuzi wa uwezo wa kuzalisha umeme wa Tanzania tangu mwaka 2013 (USAID, 2022). Mpango huo ulisaidia shirika la Serikali, TANESCO, na makampuni ya Tanzania kupitia upembuzi yakinifu, kununua vifaa na kufunga kwenye gridi ya umeme.

Kwa kushirikiana Pamoja na washirika wa Tanzania, Power Africa iliwezesha msaada wa kifedha na kiufundi (USAID, 2015) kusaidia mitambo ya Kinyerezi I (MW 150) na Kinyerezi II (MW 240) inayotumia gesi, mtambo mdogo wa kufua umeme wa mto Kiwira (MW 10) na mtambo wa umeme wa jua wa Kigoma (MW 5), miongoni mwa mingine. Kwa kuwa kaya nyingi za Kitanzania bado hazijaunganishwa kwenye gridi ya umeme, kazi ya Power Africa ya watoa huduma za umeme nje ya gridi ya taifa kama vile Devergy ni muhimu katika kusaidia kaya kubadilisha nishati ya jua kuwa chanzo cha kuaminika cha umeme wa ndani ambapo takribani uunganishaji kwa kaya milioni 2.38 umefanyika (USAID, 2019).

MCC ilishiriki katika uwekezaji wa sekta ya nishati kwa kushirikiana na washirika wa Tanzania—kupanua njia za umeme kwa kaya 337, kufadhili uunganishaji wa gharama nafuu kwa kaya maskini, kukuza uzalishaji wa umeme wa jua kupitia ufungaji wa mifumo ya photovoltaic (PV) mkoani Kigoma, kuunganisha Gridi ya umeme ya Zanzibar hadi bara, na kuboresha vituo vidogo kadhaa (MCC, n.d.; MCC, 2015; Mathematica, 2024). Tathmini huru zilizofanyika kwa miradi hiyo zinaonyesha jinsi uwekezaji wa nishati unavyoweza kutafsiriwa katika manufaa yanayoonekana kwa jamii za Kitanzania: kuongezeka kwa matumizi ya mifumo ya jua ya PV kama chanzo cha gharama nafuu cha nishati (Mathematica, 2017a); viwango vya juu vya uunganishaji, kuimarika kwa usalama wa usiku, na kupunguza viwango vya umaskini kutokana na upanuzi wa njia za umeme (Mathematica, 2017b); upanuzi wa shughuli za kujiongezea kipato kwa kutumia umeme wa gridi (Mathematica, 2017c); na ubora wa umeme miongoni mwa wafanyakazi wa hoteli na wageni kutoka kwenye kebo ya chini ya bahari hadi kisiwa cha Unguja (Mathematica, 2015).

Kielelezo Na. 14. Watanzania wenye huduma ya umeme, 2000-2021

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha asilimia ya Watanzania waliopata umeme kuanzia mwaka 2000 hadi 2021. Chanzo: Viashiria vya Maendeleo ya Dunia, Benki ya Dunia.

Kielelezo Na. 15. Uzalishaji wa umeme kwa chanzo cha mafuta nchini Tanzania, 2000-2021

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha uzalishaji wa umeme (kWh bilioni) nchini Tanzania kwa chanzo cha nishati kutoka mwaka 2000 hadi 2021. Gesi asilia imejumuishwa chini ya nishati ya masalia ya viumbe hai. Ingawa data ya msingi kutoka EIA haitofautishi kati ya gesi asilia na nishati nyinginezo, tunaweza kukadiria kiasi cha umeme kinachozalishwa na gesi asilia kwa kutumia uwiano wa uzalishaji wa umeme wa mafuta kutokana na gesi asilia. Gesi asilia inawakilisha MW 876 dhidi ya uwezo wa kuzalisha megawati 1,116 kwa ajili ya nishati ya masalia ya viumbe hai (USAID, 2019) ambayo ni asilimia 78.5 ya uwezo wa kuzalisha mafuta nchini Tanzania. Chanzo: Usimamizi wa Taarifa za Nishati (EIA).

Funzo #14. Kwa kupitia Sheria ya Ukuaji na Fursa barani Afrika, Tanzania iliongeza mauzo yake ya nguo nchini Marekani bila ushuru mara 45 kati ya mwaka 2009 hadi 2022.

Tanzania ni mtumiaji mahiri wa Sheria ya Ukuaji na Fursa ya Afrika: zaidi ya asilimia 90 ya mauzo yake ya nje kwenda Marekani (bila kujumuisha mafuta ghafi) yananufaika na uingizaji usiotozwa ushuru chini ya sheria hii (USITC, 2023; Ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, 2024). Sheria hii rafiki ilifungua njia kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuharakisha mauzo yao ya nguo kwa wateja wa Marekani mara 45 kati ya mwaka 2009 na 2022 (Kielelezo Na. 16). Tangu mwanzo, Tanzania iliimarisha ubora na wingi wa mauzo yake ya nguo, na kufikisha dola milioni 75 za bidhaa hizo nchini Marekani mwaka 2022 pekee, huku UVIKO-19 ikipunguza kwa muda mwelekeo huo wa kukua.

Serikali ya Tanzania—kulingana na Mkakati wake wa kutoka Pamba hadi Nguo wa mwaka 2016 na Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya makubaliano ya AGOA—imewekeza katika uunganishaji wa viwanda vyake vya nguo ili kuongeza usambazaji wake wa pamba ya ndani, ambayo pia imewezesha mauzo ya nje kwa nchi zaidi ya Marekani (USITC, 2023; MITI, 2016a na 2016b; Signe, 2022). Uzalishaji wa juu katika sekta hii unaweza kuleta manufaa makubwa kwa kaya, kwani wastani wa mfanyakazi wa sekta ya mavazi nchini Tanzania anakadiriwa kusaidia kifedha wanafamilia tisa (Manduna, 2024).

Kielelezo Na. 16. Biashara ya nguo ya Marekani-Tanzania, 2000-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha uwiano kati ya mauzo ya nje ya Tanzania kwenda (mstari wa bluu nyeusi) na uagizaji kutoka (mstari wa rangi ya machungwa) Marekani katika tasnia ya nguo kuanzia 2000 hadi 2022. Chanzo: World Integrated Trade Solution, Benki ya Dunia na UNCTAD.

Funzo #15. Tanzania, kwa kushirikiana na Marekani, inaendelea kustahimili VVU/UKIMWI, baada ya kutoa matibabu ya kuokoa maisha na kuepusha takribani 3/4 ya vifo zaidi ya milioni.

Afya ya watu wa Tanzania iliimarika sana kuanzia mwaka 1990 hadi 2021, kama ilivyopimwa kwa kuongezeka kwa umri wa kuishi katika miongo mitatu iliyopita (Kielelezo Na. 17). Kwa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Afya ya Tanzania, Serikali ya Marekani na mashirika yake ya uhisani binafsi yanayofanya kazi katika sekta ya afya yalisaidia kupunguza vifo vinavyotokana na visababishi mbalimbali vikiwemo VVU/UKIMWI pamoja na magonjwa ya watoto wachanga na wenye umri wa zaidi ya mwaka mmoja.

Idadi ya watu wenye afya bora huzalisha faida nyingine chanya kwa jamii ya Kitanzania kwa kiasi kikubwa. Watu wenye afya njema wana tija zaidi kwa muda mrefu katika kazi, kwani hukosa siku chache za kazi na shule, ambayo huchangia ubora wa juu wa maisha na ni faida kwa uchumi mpana. Ufikiaji wa huduma bora za afya zinaokoa na kuboresha maisha hivyo kupunguza mivutano ya kijamii kuhusu ukosefu wa usawa kati ya makundi mbalimbali.

Kielelezo Na. 17. Umri wa kuishi Tanzania baada ya kuzaliwa, 1990-2021

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha umri wa kuishi wa Watanzania baada ya kuzaliwa kuanzia mwaka 1990 hadi 2021. Chanzo: Viashiria vya Maendeleo ya Dunia, Benki ya Dunia.

Tangu kuanza kwa janga la VVU/UKIMWI, Tanzania ilipanda na kushuka kwa kasi kwa VVU nchini kote. Kati ya mwaka 1990 na 2002, vifo vya VVU/UKIMWI viliongezeka zaidi ya mara tatu (kutoka 35,000 kwa mwaka hadi 120,000/mwaka). Hata hivyo, kuanzia mwaka 2005 hadi 2022, Tanzania iliweka alama ya mabadiliko makubwa katika uwezo wake wa kupunguza idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo, na kupunguza viwango vya vifo hadi 22,000 kwa mwaka (UNAIDS, 2024).[20] Utoaji wa matibabu ya kuokoa maisha kwa dawa za kurefusha maisha (ART) tangu 2004 umekuwa sehemu muhimu ya maelezo ya mafanikio (Somi et al., 2009),[21] na kuepusha takribani vifo 778,000 nchini Tanzania hadi kufikia 2022. (Kielelezo Na. 18).[22] Asilimia ya watu wanaoishi na UKIMWI wanaopokea matibabu ya ART iliongezeka kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 94 mwaka 2022. Marekani imesaidiaprogramu za VVU nchini Tanzania tangu mwaka 2003 kwa msaada wa zaidi ya dola bilioni 6. Mwaka 2021, Marekani ilichangia asilimia 75 ya ufadhili wa programu za VVU nchini Tanzania (PEPFAR, 2021).

Afya ya watoto nchini Tanzania pia imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, na kama ilivyo kwa VVU/UKIMWI, idadi yote inakwenda katika mwelekeo sahihi. Kufikia mwaka 2021, vifo vya watoto wachanga chini ya miezi minne vilipungua hadi theluthi moja, vifo vya watoto wa mwaka mmoja na zaidi hadi mitano, na vifo vya watoto wachanga chini ya miezi minne hadi nusu ya vile ilivyokuwa mwaka 1990 (Kielelezo Na. 19).[23][24][25] Maboresho haya ya afya ya mtoto yalitokea katikati ya janga la VVU/UKIMWI, ambalo mapema lilitishia kubadili mwelekeo huo wa kushuka kutokana na maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Mipango ya fanisi ya afya, (inayoungwa mkono na msaada wa kifedha na kiufundi wa Marekani) kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kuongeza chanjo, na kuboresha lishe ya watoto wachanga, pamoja na afua zingine za afya ya mtoto zinaweza kuwa zimechangia, angalau kwa sehemu, kupata faida hizo.

Kielelezo Na. 18. Vifo vitokanavyo VVU/UKIMWI (1990-2022) vilipungua kupitia ART (2010-2022), nchini Tanzania

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha idadi ya vifo vinavyotokana na VVU/UKIMWI vya Watanzania na vifo vilivyozuiliwa kutokana na ART kuanzia mwaka 1990 hadi 2021. Chanzo: AIDSINFO, UNAIDS.

Kielelezo Na. 19. Vifo vya watoto wachanga kuanzia miaka 0-5 nchini Tanzania, 1990-2021

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha viwango vya vifo vya watoto wachanga umri wa miezi minne, watoto wachanga miezi minne hadi sita na watoto wa mwaka mmoja au zaidi wa Tanzania kuanzia mwaka 1990 hadi 2021. Chanzo: UN Inter-agency Group for Child Mortality Estimation.

Funzo #16. Marekani imesaidia elimu ya msingi nchini Tanzania kwa miongo kadhaa na elimu ya vijana inaendelea kuimarika, huku wanawake wakifaulu zaidi kuliko wanaume.

Elimu ya msingi, ikiwa ni pamoja na stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu, ni muhimu kwa watoto na vijana wa Kitanzania kushiriki kikamilifu katika jamii, kuchangia kwa tija katika uchumi, na waweze kujikimu wao na familia zao. Serikali ya Tanzania imeweka kipaumbele katika kuimarisha upatikanaji na ubora wa elimu ya msingi. Matokeo yanatia moyo: viwango vya stadi za kusoma na kuandika vimeongezeka kwa asilimia 18 kutoka mwaka 2002 hadi 2022 (Kielelezo Na. 20), huku wanawake wenye umri wa miaka 15-24 wakiwashinda wenzao wa kiume hadi kufikia 2022 katika tathmini ya endelevu.

Mashirika ya Serikali ya Marekani, mashirika yasiyo ya kiserikali, na taasisi binafsi zimeshirikiana na Serikali ya Tanzania kwa miongo kadhaa kuimarisha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto na vijana nchini Tanzania. Ufadhili kutoka Serikali ya Marekani kwa ajili ya elimu umeongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita (Kielelezo Na. 20). Usaidizi wa Marekani umeweka mkazo mahususi katika kutengeneza nyenzo za kusoma, mafunzo ya walimu, ushirikishwaji wa jamii, na miongozo kuhusu tathmini ya kusoma na kuandika.

USAID, kwa mfano, imetoa ufadhili na msaada wa kitaalamu kupitia programu kadhaa za uboreshaji. Mpango wa miaka mitano wa Tusome Pamoja (2016-21) ulilenga kuboresha matokeo ya ujifunzaji kwa madarasa ya awali, kusoma, kuandika, na kuhesabu kwa watoto milioni 1.4 katika shule zaidi ya 3,000 kwenye wilaya 42 zilizoshiriki (RTI, 2018; USAID, 2012-2017). Juhudi zinazohusiana na hizo ni kuboresha elimu ya Hesabu na Elimu Jumuishi katika wilaya hizo (RTI, 2021).

Mpango wa miaka minne wa Jifunze Uelewe (2021-2025) unasisitiza uboreshaji wa ufundishaji wa walimu na kusaidia elimu-jumuishi kwa watoto milioni 1.28 wa Morogoro, Iringa, Mtwara, Ruvuma, na Zanzibar (USAID, 2021; USAID, n.d.b.). Mnamo mwaka wa 2022, USAID ilianza kutekeleza mpango wa miaka minne wa Nahodha Kijana unaolenga uwezeshaji wa vijana kielimu, ukitoa kipaumbele kwa vijana walio nje ya shule wenye umri wa miaka 15-25 (USAID, Februari 2023).

Kielelezo Na. 20. Stadi za kusoma na Kuandika kwa vijana wa Tanzania na misaada ya kifedha ya Serikali ya Marekani katika elimu 2000-2022

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonesha viwango vya kusoma na kuandika vya vijana wa kike (machungwa) na wa kiume (bluu nyeusi) na msaada wa kifedha wa serikali ya Marekani katika elimu kuanzia mwaka 2000 hadi 2022. Chanzo: Viashiria vya Maendeleo ya Dunia, Benki ya Dunia; ForeignAssistance.gov.

Ripoti za awali za maendeleo na tathmini za matokeo ya programu hizo zinaonesha manufaa yanayoonekana kwa jamii ya Watanzania. Mpango wa Tusome Pamoja uliripotiwa kutoa mafunzo kwa walimu wa Kitanzania zaidi ya 10,000 juu ya mafunzo ya kusoma kwa darasa la awali, kusambaza vifaa vya kujifunzia milioni 1 kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili, na kusaidia vikundi 280 vya akiba vya akina mama na walezi ambavyo viliokoa karibu dola 435,000 (TZS bilioni 1) ili kuhamasisha wasichana waliobalehe kubakia shuleni (USAID, n.d.c.). Ili kuhimiza ushiriki mkubwa wa jamii katika mafanikio ya elimu ya watoto, Jifunze Uelewe ilianzisha majukwaa 2,045 ya kijamii (Ushirikiano wa Walimu wa Wazazi) ili kusaidia kutatua matatizo na kujenga ushirikiano (USAID, Februari 2023). Mpango huo pia ulisambaza nyenzo za ziada za kusoma milioni 1 kwa madarasa ya awali na kutoa mafunzo kwa zaidi ya walimu 23,000 wa Kitanzania hadi sasa katika stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu na elimu jumuishi, miongoni mwa mada nyinginezo (ibid).

4.2 Maoni ya Viongozi juu ya Ushirikiano wa Marekani na Tanzania

Katika sehemu iliyotangulia, tulijadili ushahidi unaoonesha kuwa Tanzania inapiga hatua katika vipaumbele vyake vya maendeleo katika nyanja kadhaa, na Marekani imekuwa mshirika mkuu katika jitihada hizo. Hata hivyo, hatuwezi kusema kwa uhakika jinsi michango hii inavyoonekana na kuonwa na viongozi wa umma, binafsi na asasi za kiraia wanaotunga na kutekeleza sera za maendeleo nchini Tanzania. Ili kupata uelewa mzuri zaidi, tulifanya uchunguzi[26] mtandaoni na usaili[27] na viongozi wa Tanzania kwa kutumia sampuli za utaratibu wa wawakilishi wa serikali, vyuo vikuu na taasisi za elimu, mashirika yasiyo ya kiserikali na ya kiraia, washirika wa maendeleo ambao wanafanya kazi nchini Tanzania, na sekta binafsi.

Watu mia moja thelathini na nane walishiriki kutoa maoni yao kupitia utafiti wa mtandaoni uliofanyika Januari mwaka 2024 ambapo asilimia 12.4 walitoa mrejesho. Wasailiwa waliwakilisha sekta 13 tofauti za utaalamu na kuchangia maoni yao kuhusu ushirikiano wa maendeleo nchini Tanzania na mchango wa Marekani na wadau wengine. Kielelezo Na. 21 kinatoa mchanganuo wa asilimia ya walisailiwa na kundi la wadau (yaani, aina za taasisi wanazofanyia kazi). Zaidi ya hayo, maafisa wa ngazi ya juu 12 kutoka taasisi 11 za serikali au asasi za kiraia walishiriki katika usaili wa ana kwa ana na mijadala ya vikundi lengwa ilifanyika Februari 2024.

Kielelezo Na. 21. Wajibu wa AidData 2024 Tanzania Snap Poll na kundi la wadau

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonyesha sehemu ya wasailiwa waliojitambulisha kuwa wa kikundi fulani cha washikadau. Chanzo: AidData's 2024 Tanzania Snap Poll.

Funzo #17. Marekani inatazamwa kama mshirika mkuu: Viongozi wa Tanzania wanaiona Marekani kuwa mshirika hai (asilimia 95) na kutoa mchango wa mkubwa (asilimia 96) kwa maendeleo ya nchi yao.

Asilimia tisini na tano ya waliosailiwa walieleza kuwa Marekani kwa kiasi fulani au kwa kiasi kikubwa sana inasaidia maendeleo ya Tanzania (Kielelezo Na. 22). Nchi nyingine zinazoongoza kati ya nchi na nchi ni kama vile Uingereza, Japani, Jamhuri ya Watu wa China na Uswidi pia zilitajwa mara nyingi kama washirika wa kawaida kwa sababu hawafanyi kazi kamawenzao wa Marekani. Mashirika ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), na Umoja wa Mataifa (UN) yalitajwa mara nyingi kuwa yanashiriki kikamilifu katika maendeleo ya Tanzania. Matokeo haya yanatilia mkazo umuhimu wa wafadhili kama Marekani na mataifa mengine yenye uchumi mkubwa kuunganisha rasilimali ili kuwekeza katika maeneo mbalimbali ili kupanua wigo wa kuwaunga mkono raia wa Tanzania kukuza maendeleo.

Kielelezo Na. 22. Maoni ya viongozi kuhusu viwango vya shughuli za washirika wa maendeleo nchini Tanzania

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonyesha idadi ya wasailiwa waliochagua jibu lililotolewa, ikilinganishwa na jumla ya idadi ya wasailiwa waliojibu sehemu swali: “Kwa ufahamu wako, wahusika wa nje wafuatao wanachangamoto gani katika kusaidia maendeleo ya Tanzania (k.m. kufanya uwekezaji, kutoa msaada, ubia wa udalali)?”. Chanzo: AidData's 2024 Tanzania Snap Poll.

Usaili na viongozi wa serikali ya Tanzania na mashirika ya kiraia ulishadadia maoni kwamba msaada wa Marekani unaonekana na kuthaminiwa:

"Serikali ya Marekani inachangia mashirika ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia, AfDB, UN na [Shirika la Fedha la Kimataifa] (IMF) kama mwanachama. Huwezi kuepuka Marekani; ukiepuka kupitia nchi na nchi, utawapata katika haya mashirika ya kimataifa.”—Afisa wa serikali ya Tanzania

“Msaada wa Marekani ni kila mahali; inanagusa kila sekta, kila mahali unapoenda, utaona ‘Imefadhiliwa au kwa hisani ya Watu wa Marekani’.” -Kiongozi wa asasi za kiraia Tanzania

Waliosailiwa walibainisha njia kadhaa ambazo serikali ya Marekani ilikuwa mshirika hai. Sambamba na uchambuzi wa mtiririko wa kifedha katika Sura ya 2 na 3, waliosailiwa walitaja michango ya Marekani katika afya ya wananchi (udhibiti wa malaria kupitia usambazaji wa vyandarua na unyunyiziaji wa dawa ya muda mrefu ndani), uzalishaji wa kilimo (kujenga uwezo kwa wakulima, mbegu bora), pamoja na biashara na kukuza uwekezaji. Kwa kuongezea, waliibua maeneo mengine ya manufaa ya ushirikiano, kama vile msaada wa utaalamu kutoka Marekani, kuboresha demokrasia na utawala kupitia marekebisho ya sheria na sera, usawa wa kijinsia, na uwezeshaji wa wanawake na watoto.

Ziara za viongozi wa ngazi ya juu wa kisiasa kutoka Marekani; kushirikisha viongozi wa mitaa na viongozi wa mashirika ya kiraia; na miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja (k.m., kusambaza vyandarua ili kukabiliana na malaria) ilitajwa na waliosailiwa kuwa ni yenye ushawishi katika kuinua hadhi ya ushirikiano wa maendeleo ya Marekani nchini Tanzania. Kinyume chake, wengine waliona kwamba Marekani inaweza kukuza au kutangaza zaidi msaada wake kulingana na ukubwa wa michango yake, kuwa makini zaidi katika kuchunguza juhudi za washirika wake, na kutegemea zaidi mashirika yasiyo ya kiserikali kutekeleza miradi ambayo inaweza kudhoofisha mwonekano wake. Ili kuongeza mwonekano wa michango yake katika siku zijazo, walipendekeza kuwa serikali ya Marekani inapaswa kuangalia mbali zaidi ya mitandao ya kijamii na mabango ya matangazo, ambayo yanawafikia sehemu ndogo ya idadi ya Watanzania, na kusisitiza yafanyike matukio, warsha, na kampeni zinazoshirikisha jamii za wenyeji zinazozunguka miradi husika.

Viongozi ambao walimtaja mshirika mmojawapo wa maendeleo kuwa anafanya kazi nzuri sana waliulizwa kutathmini ni kwa kiwango gani mhusika huyo alikuwa na mchango wenye manufaa kwa Tanzania. Asilimia 96 ya waliosailiwa walionyesha kuwa Marekani sio tu kwamba alikuwa mshirika hai bali ametoa "kiasi cha kuridhisha" au "mchango mkubwa" kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania. Walipoulizwa kukadiria ni kiasi gani mashirika ya Serikali ya Marekani yalichangia Tanzania kwa wastani kwa kila mwaka, asilimia 39 walidhani kwamba michango ya Marekani ilikuwa chini kuliko kiasi halisi cha msaada.[28]

Usaili wa kina ulionyesha mifano mahususi ambayo viongozi wa Tanzania waliiona kuwa ni mfano mzuri wa mafanikio ya ushirikiano wa kimaendeleo kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita. Sambamba na mjadala katika Sehemu ya 4.1, afya lilikuwa ni suala lililojitokeza mara kwa mara—kutokana na programu za kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza (k.m., VVU/UKIMWI, malaria na kifua kikuu) na kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto hadi kusambaza chakula chenye lishe bora kwa wanafunzi wa shule za msingi kupitia miradi ya lishe. Waliosailiwa waliripoti juu ya faida kubwa ya tiba ya kurefusha maisha na hatua nyingine zinazohusiana ambazo zinazoungwa mkono na serikali ya Marekani katika kusaidia kupunguza kiwango cha maambukizi ya VVU/UKIMWI kutoka tarakimu mbili hadi moja.

Waliosailiwa pia walithamini na kupongeza msaada wa chakula na kuongeza tija ya kilimo cha Tanzania na uthabiti wa mifumo yake ya chakula kukabiliana na majanga kwa siku zijazo. Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Tanzania wa Feed the Future unaotekelezwa na USAID, ulitajwa kuwa moja ya mafanikio katika kufanya kazi na wakulima wadogowadogo ili kuongeza mavuno na kipato kupitia mafunzo ya mbinu za kisasa za kilimo, kuimarisha uhusiano wa kimasoko, na shughuli nyinginezo. Sambamba na hilo, waliosailiwa pia walitaja miradi ya ASPIRES (Sera ya Kilimo na Maboresho ya Taasisi) na PS3 (Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma) kuwa ni mifano madhubuti ya mafanikio ya kuongeza tija katika kilimo na kuimarisha ushirikiano na wenzao wa Tanzania.

Kwa kulinganisha, waliosailiwa waliona kuwa msaada wa Marekani haujafanikiwa katika sekta ya migodi hasa madini. Waliona kuwa kuna changamoto kwa kiasi fulani ya miundombinu duni (k.m., barabara mbovu) na kukabiliana na mienendo hasi kutoka kwa miradi kama hiyo inayohusiana na uharibifu wa mazingira, migogoro ya kijamii, mizozo ya ardhi, na masuala mengine. Licha ya kuongezeka kwa mtiririko wa utalii, biashara na uwekezaji kati ya Marekani na Tanzania katika kipindi cha muongo mmoja uliopita (tazama Sura ya 3), wasailiwa walieleza kuwa Marekani haikujidhatiti katika kusaidia maeneo hayo, hasa katika miaka ya hivi karibuni. Pia, kwa kiasi fulani kinyume na uwekezaji wa hali ya juu wa serikali na sekta binafsi katika eneo hilo, wasailiwa walieleza kuwa Marekani imekuwa haiungi mkono sekta ya nishati katika miaka ya hivi karibuni. Wakitafakari kwa nini inaweza kuwa hivyo, walihisi kwamba hii inaweza kuwa na uhusiano na baadhi ya mivutano ya awali kati ya Washington na Dodoma kuhusu demokrasia ya Tanzania na rekodi ya haki za binadamu. Hata hivyo, waliripoti kuwa wameanza kuona mabadiliko chanya kuelekea kwenye kuongeza uungwaji mkono kwa Tanzania katika kukabiliana na juhudi zake za kuimarisha demokrasia na uhuru wa kujieleza.

Kwa kuwa Marekani sio mshirika pekee anayeendesha shughuli zake nchini Tanzania, tuliwauliza viongozi wakuu wakati wa usaili kuhusu ni kwa kiwango gani waliona serikali ya Marekani ikishirikiana na washirika wengine wa maendeleo wa nchi na nchi na kimataifa—kuanzia kubadilishana habari hadi kuunganisha rasilimali kuelekea malengo ya pamoja. Waliosailiwa waligawanyika kwa kiasi fulani katika mitazamo yao kuhusu suala hili. Kwa mujibu wa Sura ya 2, walionesha kiwango cha juu cha ufadhili wa Marekani unaotolewa kupitia mashirika ya kimataifa kama vile Mpango wa Chakula Duniani kuwa ni ishara ya uratibu wa juhudi za pamoja kukabiliana na changamoto za maendeleo ya Tanzania. Hata hivyo, kulikuwa na uhakika mdogo kuhusu uratibu wa Marekani na wafadhili wengine wa nchi na nchi. Ingawa viongozi waliripoti kwamba baadhi ya shughuli za umma zilipokea msaada wa pamoja kutoka kwa wafadhili kadhaa, baadhi yao walisema kuwa Marekani ilitaka kuweka shughuli zake tofauti ili iwe rahisi kufuatilia kwa karibu kuona jinsi msaada wao unavyotumiwa na kutathmini matokeo yake.

Funzo #18. Viongozi wa Tanzania wanaona mawanda ya serikali ya Marekani, mashirika ya kiraia, na taasisi za sekta binafsi kuwa zinafaa zaidi kutoa aina tofauti za msaada.

Wasailiwa ambao walikuwa wameitambua Marekani kama mshirika thabiti wa maendeleo waliulizwa ni aina gani ya mashirika ya Kimarekani yalikuwa yanafanya kazi katika sekta yao na kwa njia zipi. Viongozi wengi walitambua mashirika ya serikali ya Marekani kuwa yanajishughulisha kikamilifu katika kutoa msaada wa maendeleo kupitia misaada na mikopo (Jedwali la 6). Kati ya mashirika hayo, USAID na MCC yalirejelewa mara nyingi katika usaili wa mtu binafsi. Taasisi binafsi pia zilionekana kuwa na bidii katika kutoa msaada wa maendeleo kuliko shughuli zingine. Katika usaili na viongozi wakuu, baadhi ya washirika hao walitajwa kwa majina kuwa na ushawishi mkubwa, ikiwa ni pamoja na Shirikika la Bill & Melinda Gates, Shirika la Rockefeller, na Kampuni ya Ford. Taasisi za kiraia za Marekani—mashirika yasiyo ya kiserikali, vyuo vikuu, na vikundi vya wasomi—zilitambuliwa kuwa wachangiaji wakuu katika masuala ya kujenga uwezo na mafunzo.

Waliosailiwa pia walitafakari juu ya michango ya washirika hao:

"Tuna miradi mingi sana na Marekani, na asilimia 99 ya miradi inafadhiliwa na USAID kupitia mashirika ya utekelezaji kama vile NGOs za kimataifa au vyuo vikuu" - Kiongozi wa serikali ya Tanzania.

"Washirika wa Marekani wametoa msaada mkubwa. Ni muhimu kutathmini michango yao kwa msaada wa jumla uliopokelewa na nchi ili kupima ukubwa wa msaada wao." -Kiongozi wa asasi za kiraia Tanzania

“Mashirika ya Marekani yameanzisha maabara nyingi ndani ya taifa hili, hasa kusaidia Idara ya Bohari ya Dawa (MSD) katika kuimarisha msururu wa ugavi. Matokeo yake ni dhahiri, kama inavyoonekana katika kuongezeka kwa umri wa kuishi nchini Tanzania kutokana na kuboreshwa kwa mfumo wa huduma za afya.” -Kiongozi wa asasi za kiraia Tanzania

Sekta binafsi ya Marekani ilitazamwa na viongozi wakuu kuwa ina msaada katika ukuaji na maendeleo ya Tanzania, hivyo kuchochea makampuni ya ndani kukua kwa kutoamafunzo juu ya mbinu zinazoendeshwa na teknolojia, na fedha za kianzio. Kampuni za bidhaa za walaji za Marekani kama vile Coca-Cola, Vodacom, na Kentucky Fried Chicken zilitambuliwa kuwa zina ushawishi zaidi kwa michango yao katika utengenezaji wa nafasi za ajira, mapato ya kodi, na uwekezaji mwingine wenye faida maradufu. Uwezo wa utafiti na maendeleo pia ulitambuliwa kuwa ni muhimu.

"Sekta binafsi ya Marekani ina jukumu muhimu katika kusaidia ukuaji na maendeleo ya Tanzania. Pia, makampuni ya Marekani yameajiri watu wengi nchini. Aidha ... sekta binafsi ya Marekani imesaidia mipango na programu za jamii katika huduma za kijamii." - Afisa wa serikali ya Tanzania.

“[Kampuni] kama Coca-Cola katika uchumi inashawishi hata kampuni za ndani kukua; sasa tuna Mo Cola, Jambo Cola ambayo ni mifano halisi ya athari za kuwa na Coca-Cola nchini.” -Kiongozi wa asasi za kiraia Tanzania

Jedwali La. 6. Maoni ya viongozi kuhusu mashirika na michango yake katika maendeleo ya Tanzania

Dokezo: Asilimia hizi zinarejelea idadi ya wahojiwa waliochagua jibu lililotolewa ikilinganishwa na jumla ya idadi ya wasailiwa waliojibu kwa kila aina ya shirika katika swali: "Ni aina gani za shughuli za mashirika haya zilichangia zaidi maendeleo ya Tanzania?". Wasailiwa waliweza tu kuchagua aina moja ya shughuli kwa kila aina ya shirika. Wasailiwa waliwasilishwa tu na aina ya shirika ikiwa hapo awali walikuwa wametambua kwamba aina ya shirika ilichangia kikamilifu maendeleo ya Tanzania. Chanzo: AidData's 2024 Tanzania Snap Poll.

Kwa kuzingatia mawanda na kutofautiana kwa wachangiaji wa maendeleo, tuliwauliza viongozi wakuu kutathmini kiwango ambacho wanaiona Serikali ya Marekani ikiratibu juhudi zake na wadau wa sekta binafsi wa Marekani. Waliosailiwa walikuwa na maoni yanayotofautiana kuhusu suala hilo. Baadhi ya viongozi waliiona serikali ya Marekani na wadau wa sekta binafsi wanatofautiana katika kuleta nguvu na rasilimali zao wakati wangeweza kuleta kwa njia zinazokamilishana. Mfano mmoja ulitolewa kutoka sekta ya afya, ambapo mipango inayoongozwa na Serikali ya Marekani kama vile Mpango wa Dharura wa Rais wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) unasaidia mipango ya VVU/UKIMWI na utambuzi wa TB, matibabu na matunzo, wakati Shirika la Gates likiwezesha upatikanaji wa tiba ya kurefusha maisha (ART) na kuimarisha maabara za utafiti wa TB na maabara za maendeleo.

Kinyume chake, biashara ya kilimo ilikuwa eneo ambalo waliosailiwa waliona kwamba kulikuwa na ushirikiano mdogo kati ya sekta binafsi ya Marekani na watendaji wa serikali kwa kushughulikia maeneo yanayotofautiana. Wakati makampuni ya Marekani yakilenga usindikaji wa chakula na uendelezaji wa mnyororo wa thamani, juhudi za serikali ya Marekani ni kusaidia usalama wa chakula na kilimo endelevu.

Funzo #19. Viongozi wa Tanzania wanaichukulia Marekani kuwa mshirika wa kutegemewa (asilimia 93) na wanaona msaada kutoka kwa mashirika ya Marekani kama nyenzo kuu ya kuimarisha ushirikiano wao (asilimia 87)

Jambo moja ambalo ni wazi kwa mshirika wa maendeleo ni kuonekana kuwa anatoa fedha nyingi au msaada wa hali na mali, lakini ni kwa kiwango gani inatazamwa kuwa ina nguvu za kuendelea kudumishwa? Wasiwasi unaooneshwa na viongozi wa mataifa ya Kusini mara nyingi katika uhusiano wao na washirika wa maendeleo ni uhakika wa ufadhili na msaada. Hata hivyo, kwa upande wa ushirikiano wa Marekani na Tanzania, matumaini ni makubwa. Asilimia 93 ya waliosailiwa walisema kwamba Marekani ni mshirika wa kutegemewa kwa kiasi au wa kutegemewa sana katika maendeleo ya Tanzania, ikilinganishwa na washirika wengine.

Hata hivyo, hiyo haimaanishi kwamba viongozi wa Tanzania wanauona ushirikiano wao na Marekani kuwa tuami. Katika baadhi ya maeneo, waliosailiwa waliona kwamba msaada wa maendeleo wa Marekani umebadilika ili kukabiliana na changamoto mpya katika mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa au UVIKO-19. Baadhi ya viongozi waligusia ustahimilivu wa hali ya hewa kama msisitizo unaoongezeka katika msaada wa kilimo wa Marekani, pamoja na kusisitiza uimarishaji wa mifumo ya afya (hasa kujiandaa kukabiliana na majanga katika sekta ya afya). Wengine walikiri kuwa mabadiliko katika uhusiano wa nchi hizo mbili yanaweza kuathiri ushirikiano wa maendeleo, kwa mfano wasiwasi wa awali wa Marekani kuhusu hali mbaya ya utawala nchini Tanzania ambao ulisababisha MCC kusitisha shughuli zake mwaka 2016, hadi iliporejesha mwaka 2023.

"Hapa kumekuwa na mabadiliko madogo kutokana na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye kilimo. Msisitizo ulibadilishwa ili kusaidia hatua za kukabiliana na hali ya hewa. ... Msaada wa sekta binafsi wa Marekani kwa ukuaji na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini Tanzania umepitia mabadiliko makubwa kwa vipindi mbalimbali, ikiakisi mabadiliko katika vipaumbele, mbinu, na sababu za nje ya Tanzania. Imebadilika kuelekea kwenye mbinu mpya zinazotumia teknolojia. -Kiongozi wa asasi za kiraia Tanzania

“Awamu ya kwanza ya MCC ilikamilika, lakini awamu ya pili, iliyokuwa na ruzuku ya karibu dola nusu bilioni, haikuanza kabisa kwa sababu ya changamoto za utawala zilizojitokeza… Hata hivyo,….. MCC inarudi na majadiliano na usanifu umeshakamilika….. kurejesha ushirikiano].” -Kiongozi wa asasi za kiraia Tanzania

Ufadhili wa nje wa miradi ya maendeleo unaweza kuhusisha hatua za usawazishaji kwa kutoa msaada mkubwa kwa namna ambayo haidhoofishi uaminifu wa ndani. Kwa upande wa Marekani, viongozi wa Tanzania waliona kuna uwezekano wa kuwa na ushirikiano rafiki na mashirika ya Marekani. Walipoulizwa maoni yao kuhusu mradi hewa uliofadhiliwa na shirika lenye makao yake nchini Marekani, asilimia 87 ya wasailiwa walisema kwamba hiyo ingesaidia juhudi za maendeleo kuwa za kuaminika zaidi mbele yao (Mchoro 23). Kwa kulinganisha, ni watu wachache (asilimia 13) waliona ufadhili wa Marekani unadhoofisha utekelezaji wa mradi.

Kielelezo Na. 23. Maoni ya viongozi kuhusu kushirikiana na Marekani na uaminifu unaohusishwa nao

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonyesha majibu ya swali: “Ikiwa utapata mradi wa maendeleo unaofadhiliwa na shirika lililoko Marekani, je, ungeuchukulia mradi huo wa kuaminika zaidi, kidogo, au wa kuaminika zaidi kuliko ukiendeshwa na shirika lenye makao yake makuu nchini Tanzania?” Chaguo za majibu "Inaaminika" na "Inaaminika zaidi" ziliunganishwa kuwa "Inayoaminika Zaidi" katika uchanganuzi. Chaguo za majibu "Isiyoaminika sana" na "Inayoaminika kidogo" ziliunganishwa kuwa "Isiyoaminika" katika uchanganuzi. Chanzo: AidData's 2024 Tanzania Snap Poll.

Funzo #20. Msaada wa Marekani unaonekana kuwa wa maana zaidi pale unapoziba pengo kubwa ambalo lipo juu ya uwezo wa Tanzania na unaoendana na dira ya maendeleo ya Taifa.

Viongozi walioyatambua mashirika ya Marekani kuwa yanachangia maendeleo nchini Tanzania walitakiwa kubainisha sababu tatu kwa nini hali hiyo ilikuwa hivyo. Washiriki wa utafiti kwa ujumla waliona jukumu la afua za maendeleo za Marekani zinakuwa na manufaa pale zinaposaidia serikali kufikia malengo yake yenyewe, kutoa msaada wa ziada ili kuziba pengo (asilimia 73) na kuoanisha kazi zao na ajenda ya maendeleo ya Tanzania (asilimia 69) (Kielelezo Na. 24). Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 ni rejea muhimu kwa viongozi wa Tanzania, na wanatambua kwamba Marekani inajaribukuendana na ajenda hiyo. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wakuu wangependa kuona msisitizo mkubwa unawekwa kwenye vipaumbele vya serikali hasa ujenzi wa miundombinu endelevu.

Kielelezo Na. 24. Maoni ya viongozi kuhusu shughuli za Marekani zinazochangia maendeleo ya Tanzania

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonyesha majibu ya swali: “Unadhani ni kwa nini shughuli hizi zilichangia maendeleo ya Tanzania?”. Waliojibu walichagua hadi chaguo 3 za majibu. Chanzo: AidData's 2024 Tanzania Snap Poll.

Waliosailiwa walithibitisha kuwa Tanzania inanufaika kwa kushirikiana na Marekani kwa njia nyingi, ikiwa ni pamoja na msaada wa kifedha, fursa za biashara, upatikanaji wa teknolojia na FDI kutoka kwa makampuni ya Marekani. Mbali na maoni hayo, viongozi wakuu pia waligusia faida zingine zisizoonekana kutokana na nafasi ya Marekani katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki za binadamu, utawala bora, na maswala ya mazingira. Ushawishi mpana zaidi wa Marekani na nguvu za kiuchumi pia zilionekana kuwa za thamani kwa washirika wake.

"Kuna faida nyingi sana za kushirikiana na Marekani… Ni rahisi kuwa na kiti katika mazungumzo ya kimataifa." -Kiongozi wa asasi za kiraia Tanzania

Hata hivyo, viongozi wa Tanzania pia wanasema kuwa ushirikiano wao na Marekani una mapungufu yake. Mojawapo ya changamoto za kawaida zilizoripotiwa ni ya ufuatiliaji na uratibu wa fedha za Marekani. Ugumu unatokana na ukweli kwamba misaada mingi ya serikali ya Marekani inatolewa kupitia sekta mbalimbali za kibinafsi na mashirika ya kiraia. Hata hivyo, Changamoto hizo si za Marekani pekee, kwani wafadhili wengine pia tunapambana na suala hilo. Changamoto nyingine za ushirikiano zinazohusiana na mienendo ya mabadiliko ya nguvu (power dynamics) na utamaduni, hasa kuepuka utegemezi, ushirikiano usio na usawa, au programu zisizo endelevu ambazo zinategemea watekelezaji wa Marekani peke yake kwa msaada wa muda mfupi.

Mhojiwa mmojawapo alihoji:

"Wakati mataifa mengine yanafadhili miradi mikubwa ya maendeleo, Wamarekani wamekuwa wakitoa misaada rahisi inayosababisha Tanzania kuendelea kuwa tegemezi kwao." -Kiongozi wa serikali ya Tanzania

Funzo #21. Takriban asilimia 60 au zaidi ya viongozi wa Tanzania waliona msaada wa Serikali ya Marekani unaisaidia nchi kuimarika katika viashiria muhimu vya uchumi, mazingira na utawala.

Viongozi wa Tanzania walidhihirisha kiwango ambacho wanaona serikali ya Marekani inasaidia kuboresha hali ya uchumi, mazingira na utawala katika nchiya. Washiriki wa utafiti walionyesha kuishukuru Marekani kwa mchango wake katika kuboresha hali ya uchumi nchini Tanzania—wastani wa asilimia 66 ya waliohojiwa walisema kuwa Marekani imeboresha hali ya uchumi kwa mujibu wa viashiria 7 (Kielelezo Na. 25). Pia, zaidi ya asilimia 70 ya viongozi walikuwa na maoni chanya kuhusu msaada wa Serikali ya Marekani katika maeneo manne: uzalishaji wa nafasi za kazi za ndani (asilimia 82), mafunzo ya ufundi na elimu (asilimia 75), mtiririko wa biashara na utalii (asilimia 73), na uboreshaji wa teknolojia na utaalamu ili kuingia katika sekta mpya (asilimia 71).

Kielelezo Na. 25. Maoni ya viongozi kuhusu michango ya Marekani katika maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonyesha majibu ya swali: “Je, msaada wa serikali ya Marekani kwenye miradi ya maendeleo nchini Tanzania umefanya mambo kuwa bora zaidi, mabaya zaidi, au hayakuwa na athari kwa uchumi katika maeneo yafuatayo?”. machaguo ya majibu "Bora" na "bora zaidi" ziliunganishwa kuwa "Bora" katika uchanganuzi. Machaguo ya majibu "Mbaya" na "mbaya zaidi" ziliunganishwa kuwa "Mbaya" katika uchanganuzi. Chanzo: AidData's 2024 Tanzania Snap Poll.

Wasailiwa waliishukuru pia Marekani kwa michango ya kuboresha utawala[29] (Kielelezo Na. 26) na hali ya mazingira[30] nchini Tanzania (Kielelezo Na. 27). Katika kuunga mkono utawala bora, viongozi mara nyingi walitaja mchango wa Marekani katika kuisaidia Tanzania kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za umma (asilimia 71) na kuhakikisha kuwepo kwa nafasi ya kiraia, ushiriki wa vikundi vya kiraia (asilimia 66), uhuru wa vyombo vya habari (asilimia 66), na upatikanaji wa haki (asilimia 65). Linapokuja suala la ulinzi wa mazingira, wahojiwa waliangazia maboresho katika matumizi endelevu ya maliasili (asilimia 70) na kupunguza uwezekano wa kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi (asilimia 66) kuwa ni michango ya Marekani.

Kielelezo Na. 26. Maoni ya viongozi kuhusu michango ya Marekani katika utawala nchini Tanzania

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonyesha majibu ya swali: “Je, msaada wa serikali ya Marekani kwa miradi ya maendeleo nchini Tanzania umefanya mambo kuwa bora zaidi, mabaya zaidi, au hayakuwa na athari kwa utawala katika maeneo yafuatayo?”. machaguo ya majibu "Bora zaidi" na "bora" yaliunganishwa kuwa "Bora" katika uchanganuzi. Machaguo ya majibu "Mbaya zaidi" na "mbaya" yaliunganishwa kuwa "Mbaya" katika uchambuzi. Chanzo: AidData's 2024 Tanzania Snap Poll.

Kielelezo Na. 27. Maoni ya viongozi kuhusu mchango wa Marekani katika mazingira nchini Tanzania

Dokezo: Kielelezo hiki kinaonyesha majibu ya swali: “Je, msaada wa serikali ya Marekani kwa miradi ya maendeleo nchini Tanzania umefanya mambo kuwa bora zaidi, mabaya zaidi, au hayakuwa na athari kwa mazingira katika maeneo yafuatayo?”. machaguo ya majibu "Bora zaidi" na "bora" yaliunganishwa kuwa "Bora" katika uchanganuzi. Machaguo ya majibu "Mbaya zaidi" na "mbaya" yaliunganishwa kuwa "Mbaya" katika uchanganuzi. Chanzo: AidData's 2024 Tanzania Snap Poll.

Sura 5: Hitimisho

Tulianza ripoti hii kwa swali: Je, Watanzania na Wamarekani wanawezaje kutathmini thamani ya ushirikiano wa nchi zao?

Katika Sura ya 2, tulikadiria kuwa Serikali ya Marekani hutoa dola bilioni 1 kila mwaka kupitia misaada rasmi ya maendeleo kwa makubaliano ya nchi na nchi—ikijumuisha ruzuku, mikopo ya masharti nafuu na ushauri wa kiufundi—pamoja na msaada unaotolewa kupitia mashirika ya kimataifa (k.m., mashirika ya Umoja wa Mataifa, benki za maendeleo) na fedha za wafadhili zinazofanya kazi nchini Tanzania. Pia, tulijaribu kubainisha jinsi sera nzuri za biashara za Marekani zinavyoisaidia Tanzania kupiga hatua kwa kasi kuelekea kuendeleza na kukuza uchumi wa kisasa.

Katika Sura ya 3, tuliweka bayana ziada ya dola bilioni 1.8 kila mwaka kwa thamani inayotokana na kukua kwa uhusiano kati ya watu na watu, makampuni, mashirika na watu binafsi kati ya Tanzania na Marekani. Uchumi wa Tanzania unanufaika na makampuni ya Marekani yanayowekeza mitaji, kutengeneza nafasi za ajira na kununua bidhaa na huduma. Mashirika ya misaada ya Marekani yanasaidia matumizi ya serikali na kuijengea uwezo Tanzania kwa kutumia fedha za sekta binafsi huku mashirika yasiyo ya kiserikali ya Marekani yanatekeleza miradi inayoboresha maisha ya kila siku ya Watanzania. Zaidi ya hayo, mapato kutoka kwa watalii wa Marekani, na fedha zinazotumwa na Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini Marekani zote zinafaidisha uchumi wa Tanzania. Kwa jumla, tunakadiria kuwa ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania huzalisha jumla ya takribani dola bilioni 2.8 kila mwaka ili kusaidia ukuaji na ustawi wa Tanzania.

Katika Sura ya 4, tulibainisha jinsi msaada wa Marekani unavyoweza kuisaidia Tanzania kupiga hatua katika malengo yake ya kiuchumi, utawala bora na mazingira kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Tuligundua kuwa viongozi wengi wa Tanzania waliosailiwa waliiona Marekani kuwa inashiriki kikamilifu na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania. Ingawa ushirikiano haukosi changamoto, kwa ujumla manufaa ya kushirikiana na Marekani yanathaminiwa.

Kwa kuzingatia changamoto za kupata takwimu kutokana na uwekezaji usio rasmi na mtiririko wa fedha, kiasi katika ripoti hii ni makadirio ya chini, na mchango wa jumla wa Marekani katika ukuaji na maendeleo ya Tanzania ama kwa hakika unaweza kuwa mkubwa zaidi. Hata hivyo, ni matumaini yetu kwamba ripoti hii imeweka msingi muhimu kwa raia na viongozi wa Tanzania kujitathmini wenyewe kuhusu thamani inayotokana na ushirikiano wa nchi yao na Marekani

Marejeleo

ACDIVOCA. (n.d.). Feed the Future Tanzania NAFAKA II Activity. https://www.acdivoca.org/projects/tanzania-nafaka-ii-cereals-market-system-development/

AfDB. (n.d.). Power Africa Initiative. https://www.afdb.org/en/topics-and-sectors/initiatives-partnerships/power-africa-initiative

Afrobarometer. (2021). In Tanzania, China outranks U.S. as positive influence and development model, Afrobarometer survey shows. https://www.afrobarometer.org/articles/tanzania-china-outranks-us-positive-influence-and-development-model-afrobarometer-survey-shows/

AidData. (2023). Global Chinese Development Finance Dataset, Version 3.0. Retrieved from https://www.aiddata.org/data/aiddatas-global-chinese-development-finance-dataset-version-3-0

BBC. (May 23 2023). Tanzania country profile. https://www.bbc.com/news/world-africa-14095776

BEA. (2023). Direct Investment by Country and Industry, 2022. U.S. Bureau of Economic Analysis. https://www.bea.gov/news/2023/direct-investment-country-and-industry-2022

Bishoge, O,K, Zhang L., Mushi, W.G., Suntu, S.L., & Mihuba, G.G. (2018). An overview of the natural gas sector in Tanzania. Journal of Applied and Advanced Research. 3(4):108-118. https://updatepublishing.com/journal/index.php/jaar/article/view/6765

Burgess, B. and Custer, S. (2023). Catalytic Partnerships: Opportunities and Challenges in Mobilizing U.S. Private Sector Resources to Scale America’s Contribution to Development Overseas. https://www.aiddata.org/publications/catalytic-partnerships-opportunities-and-challenges-in-mobilizing-u-s-private-sector-resources-to-scale-americas-contribution-to-development-overseas

Christopher, J. (October 2023). Tanzania targets $15 Billion annual FDI by 2025, says President Samia. The Citizen. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/business/tanzania-targets-15-billion-annual-fdi-by-2025-says-president-samia-4396986

Cooke, J. and Hubner, B. (May 2016). Tanzania's Ruptured Relationship with the Millennium Challenge Corporation https://www.csis.org/analysis/tanzanias-ruptured-relationship-millennium-challenge-corporation

DFC. (n.d.a). Public Information Summary - Tanzania - CRDB Bank Plc. https://www.dfc.gov/sites/default/files/media/documents/9000104763.pdf

DFC. (n.d.b). Public Information Summary - Tanzania -First Housing Finance (Tanzania) Ltd. (“FHF”). https://www.dfc.gov/sites/default/files/media/documents/9000115875.pdf

DOD. (March 2023). Department of Defense Drug Interdiction and Counter‐Drug Activities: Fiscal Year 2024 Budget Estimates). https://comptroller.defense.gov/Portals/45/Documents/defbudget/FY2024/FY2024_Drug_Interdiction_and_Counter-Drug_Activities.pdf

DOL. (n.d.) WEKEZA: Wezesha Ustawi, Endeleza Kiwango cha Elimu Kuzia Ajira kwa Watoto/ INVEST: Supporting Livelihoods and Developing Quality Education to Stop Child Labor. Bureau of International Labour Affairs, U.S. Department of Labor. https://www.dol.gov/agencies/ilab/wekeza-wezesha-ustawi-endeleza-kiwango-cha-elimu-kuzia-ajira-kwa-watoto-invest

ESI Africa. (September 2014). Symbion Power commits US$900m to Tanzania gas to power plant. https://www.esi-africa.com/top-stories/symbion-power-commits-us900m-to-tanzania-gas-to-power-plant/

fDi Marketplace. (2024). The Financial Times Ltd.

Gavin, M. (May 2022). A Stronger U.S.-Tanzania Relationship Would Be Mutually Beneficial. Council on Foreign Relations. https://www.cfr.org/blog/stronger-us-tanzania-relationship-would-be-mutually-beneficial

Gordon, K. (2008). Investment Guarantees and Political Risk Insurance: Institutions, Incentives and Development. OECD. https://www.oecd.org/finance/insurance/44230805.pdf

IBAR. (n.d.). Communiqué - Workshop on the Establishment of the East Africa Platform of Non State Actors in Fisheries and Aquaculture Sector (EARFISH). Inter African Bureau for Animal Resources, African Union. https://www.au-ibar.org/node/232

IBAR. (May 2015). Livestock vaccination campaign along Kenya- Tanzania border bears fruit. Inter African Bureau for Animal Resources, African Union. https://www.au-ibar.org/au-ibar-news/livestock-vaccination-campaign-along-kenya-tanzania-border-bears-fruit

John Snow Inc. (2016). USAID DELIVER PROJECT Final Country Report Tanzania. https://deliver.jsi.com/wp-content/uploads/2016/12/FinaCounRepo_TZ.pdf

Maduna, C. (Jan. 31, 2024). AGOA Renewal: Committing to Trade and Development in Africa. https://www.iatp.org/agoa-renewal-trade-and-development-africa

Mathematica. (2015). Evaluation of the Zanzibar Interconnector Activity: Findings from the Hotel Study. https://www.mathematica.org/publications/evaluation-of-the-zanzibar-interconnector-activity-findings-from-the-hotel-study

Mathematica. (2017a). Grid Electricity May Curb Poverty in Tanzania, but Connection Rates Remain Low. https://www.mathematica.org/news/grid-electricity-may-curb-poverty-in-tanzania

Mathematica. (2017b). Grid Electricity May Curb Poverty in Tanzania, but Connection Rates Remain Low. https://www.mathematica.org/news/grid-electricity-may-curb-poverty-in-tanzania

Mathematica. (2017c). Impacts of New Electric Line Extensions in Tanzania (In Focus Brief). https://www.mathematica.org/publications/impacts-of-new-electric-line-extensions-in-tanzania-in-focus-brief

Mathematica. (2024). Tanzania Energy-Sector Impact Evaluation. https://www.mathematica.org/projects/tanzania-energy-sector-evaluation

MCC. (n.d.). Tanzania Compact. Washington, DC. MCC. (n.d.). Tanzania Compact. Washington, DC. https://www.mcc.gov/where-we-work/program/tanzania-compact/

MCC. (n.d.). Tanzania Compact. Washington, DC. https://www.mcc.gov/where-we-work/program/tanzania-compact/

MCC. (2015). Closed compact report: Tanzania Compact. https://www.mcc.gov/resources/doc/closed-compact-report-tanzania/#

MCC. (November 2015). Closed compact report: Tanzania Compact.https://assets.mcc.gov/content/uploads/closed-compact-report-tanzania.pdf

MCC. (February 2024). Millennium Challenge Corporation Deputy CEO Chidi Blyden Advances Threshold Partnerships in Tanzania and Kenya. https://www.mcc.gov/news-and-events/release/release-022024-mcc-deputy-ceo-visits-tanzania-and-kenya/

MIGA. (n.d.). Silverlands Tanzania Limited. https://www.miga.org/project/silverlands-tanzania-limited

Ministry of Finance and Planning, Tanzania. (Jun. 2021). FYDP III - National Five Year Development Plan 2021/22 - 2025/26. https://www.tro.go.tz/wp-content/uploads/2021/06/FYDP-III-English.pdf

Ministry of Industry, Trade and Investment (MITI), Tanzania. (2016a). United Republic of Tanzania Cotton-to-Clothing Strategy, 2016-2020. https://khoyout.com/ar/files/20528.pdf

MITI, Tanzania. (2016b). Tanzania National AGOA Strategy. https://agoa.info/images/documents/6213/tanzania-agoa-strategy-final.pdf

National Bureau of Statistics, Tanzania. (n.d.). The 2022 International Visitors’ Exit Survey Report. https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/Tourism/2022_International_Visitors_Exit_Survey_Report.pdf

Office of U.S. Trade Representative. (2024). African Growth and Opportunity Act (AGOA). https://ustr.gov/issue-areas/trade-development/preference-programs/african-growth-and-opportunity-act-agoa

Okafor, C. (September 2023). Top 10 African countries with the largest foreign investments. Business Insider Africa. https://africa.businessinsider.com/local/lifestyle/top-10-african-countries-with-the-largest-foreign-investments/cysb3ch

Planning Commission, Tanzania. (Jan. 1999). The Tanzania Development Vision 2025. http://www.tzonline.org/pdf/theTanzaniadevelopmentvision.pdf

PEPFAR. (2022). Appendix II: Estimated budgetary contribution to HIV/AIDS efforts by major funders for Fiscal Year 2021. https://www.state.gov/wp-content/uploads/2023/01/Tab-3-Appendix-II.2022.pdf

PMI VectorLink. (August 2022). U.S. President’s Malaria Initiative VectorLink Tanzania. https://pmivectorlink.org/wp-content/uploads/2022/08/PMI-VectorLink-Tanzania-Fact-Sheet.pdf

RTI. (2018). USAID Tusome Pamoja: Annual Report-Final Approved: October 1, 2017 to September 30, 2018. https://pdf.usaid.gov/pdf_docs/PA00TQHD.pdf

RTI. (2021). USAID Hesabu na Elimu Jumuishi (Arithmetic and Inclusive Education): Quarter 2 Progress Report: January 1, 2021, through March 31, 2021. https://pdf.usaid.gov/pdf_docs/PA00XGMB.pdf

Security Assistance Monitor. (2020). Security Assistance Monitor Map. https://securityassistance.org/map/

Signe, L. (June 16, 2022). African Growth and Opportunity Act (AGOA): Program Usage, Trends and Sectoral Highlights. www.brookings.edu/wp-content/uploads/2022/08/Testimony-Landry-Signe-June-9-2022.pdf

Somi, G., Matee, M., Makene, C.I., Van Den Hombergh, J., Kilama, B., Yahya-Malima, K.I., Masako, P., Sando, D., Ndayongeje, J., Rabiel, B., & Swai, R.O. (Jul. 2009). Three years of HIV/AIDS care and treatment services in Tanzania: achievements and challenges. Tanzania Journal Health Research. 11(3):136-43. https://www.ajol.info/index.php/thrb/article/view/47700

Statistia. (n.d.). Value of remittances sent from/to Tanzania to/from other countries or territories worldwide in 2021. https://www.statista.com/statistics/1382958/bilateral-remittances-tanzania/

Symbion Power. (n.d.a). Ubungo, Dodoma and Arusha Power Plants | 225 MW. https://www.symbion-power.com/tanzania/

Symbion Power. (n.d.b). The MCC National Distribution Project. https://www.symbion-power.com/tanzania-td/

TanzaniaInvest. (2023). Power: Tanzania Energy Mix 2023. https://www.tanzaniainvest.com/power#:~:text=Tanzania%20is%20endowed%20with%20diverse,as%20of%2031st%20December%202023

Tanzania Investment Center. (2015). Why Invest In Tanzania? An Overview of Investment Climate, Opportunities, Trends & Services Provided by Tanzania Investment Centre. https://www.fr.tzembassy.go.tz/uploads/Why_Invest_in_Tanzania.pdf

The Citizen. (November 2023). Direct flights between Tanzania and United States to begin 2024. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/national/direct-flights-between-tanzania-and-united-states-to-begin-2024--4429152

The East African. (December 2023). MCC Returns to Tanzania after 7-year Absence. https://www.theeastafrican.co.ke/tea/business/mcc-returns-to-tanzania-after-7-year-absence-4472852#google_vignette

Travel Agent Central. (April 2022). Tanzania’s President Launches “Royal Tour” in New York. https://www.travelagentcentral.com/destinations/tanzanias-president-launches-royal-tour-new-york

UNAIDS. (2024). AIDSINFO: Global data on HIV epidemiology and response. https://aidsinfo.unaids.org/

UNCTAD. (n.d.). World Investment Report 2023. https://unctad.org/publication/world-investment-report-2023

USAID. (n.d.a.). East Africa Trade and Investment Hub Fact Sheet. https://www.usaid.gov/document/east-africa-trade-and-investment-hub-fact-sheet

USAID. (n.d.b.). The United States Government Launches Jifunze Uelewe, a Four-and-a-Half-Year Education Activity to Benefit More than 1.2 Million Children. https://www.usaid.gov/tanzania/press-release/united-states-government-launches-jifunze-uelewe-four-and-half-year-education-activity-benefit-more-12-million-children

USAID. (n.d.c.). Tanzania: Education. https://www.usaid.gov/tanzania/education#:~:text=Although%20Tanzania%20has%20made%20progress,early%20grades%20read%20 with%20 comprehension

USAID. (2012-2017). Tanzania: Education. https://2012-2017.usaid.gov/tanzania/education

USAID. (2015) What Power Africa Means for Tanzania. www.usaid.gov/sites/default/files/2022-05/Tanazania%20Country%20Fact%20Sheet__05_04_15.pdf

USAID. (October 31, 2016). Caring for Children and Empowering Young People (C2EYP) Project: Quarterly Progress Report for Project Year 2016, Quarter 4. https://pdf.usaid.gov/pdf_docs/PA00XVKR.pdf

USAID. (February 2017). East Africa Trade and Investment Hub. https://www.usaid.gov/sites/default/files/2022-05/EATIH_fact_sheet_A4_February_2017.pdf

USAID. (2019) Tanzania, Power Africa fact sheet. https://www.usaid.gov/powerafrica/tanzania

USAID. (May 2022). Power Africa Annual Report 2021. https://www.usaid.gov/sites/default/files/2022-05/2021-Power-Africa-Annual-Report.pdf

USAID. (June 2021). Tanzania: Jifunze Uelewe - Fact Sheet. https://www.usaid.gov/sites/default/files/2023-04/Jifunze_Uelewe_Fact_Sheet_English_Final%20%282%29.pdf

USAID. (August 2022). Agriculture Tanzania Fact Sheet. https://www.usaid.gov/sites/default/files/2022-12/Agriculture_Fact_Sheet.pdf

USAID. (October 2022). Data-Driven Advocacy Tanzania Fact Sheet. https://www.usaid.gov/sites/default/files/2022-12/DDA_Fact_Sheet..._1.pdf

USAID. (2022a). East African Community Fact Sheet. https://www.usaid.gov/sites/default/files/2022-05/EAC_Fact_Sheet_2022.pdf

USAID. (January 2023). Tanzania Activity Briefer January 2023. https://www.usaid.gov/sites/default/files/2023-04/FINAL_USAID_Tanzania_Activity_Briefer_January_2023.docx.pdf

USAID. (February 2023). Tanzania Education Fact Sheet. https://www.usaid.gov/sites/default/files/2023-03/Tanzania%20Education%20Fact%20Sheet%20-%20Jan%202023..pdf

U.S. Department of State. (June 2015). Tanzania Investment Climate Statement 2015. https://2009-2017.state.gov/documents/organization/244606.pdf

U.S. Embassy in Italy. (n.d.). Senior Biden officials deepen ties in visits to Africa. https://it.usembassy.gov/senior-biden-officials-deepen-ties-in-visits-to-africa/

U.S. Embassy in Tanzania. (Feb. 3, 2023). US & Tanzania Commemorate 20 Years of PEPFAR Achievements & Success in the Fight Against HIV/AIDS. https://tz.usembassy.gov/20-years-of-pepfar-achievements/

U.S. Embassy in Tanzania. (Oct. 26, 2023). USAID’s Project Enhances Tanzania’s Capacity to Deliver Quality Mother to Child Prevention & Care Services. https://tz.usembassy.gov/usaids-project-enhances-tanzanias-capacity-to-deliver-quality-mother-to-child-hiv-prevention-and-care-services/

U.S. International Trade Administration (USITA). (Dec. 12, 2022). Tanzania - Country Commercial Guide. https://www.trade.gov/country-commercial-guides/tanzania-energy

U.S. International Trade Commission (USITC). (June 2023). African Growth and Opportunity Act (AGOA): Program Usage, Trends, and Sectoral Highlights. www.usitc.gov/publications/332/pub5419.pdf

U.S. Relations with Tanzania. Bilateral Relations Fact Sheet. Bureau of African Affairs. US Department of State. Updated: August 10, 2023. Retrieved from: https://www.state.gov/u-s-relations-with-tanzania/

Wilson Center. (April 2022). A New Day for U.S.-Tanzania Relations: A Conversation with H.E. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania. https://www.wilsoncenter.org/event/new-day-us-tanzania-relations-conversation-he-samia-suluhu-hassan-president-united-republic

World Bank Group. (July 2021). Transforming Tourism : Toward a Sustainable, Resilient, and Inclusive Sector (English). Washington, D.C. http://documents.worldbank.org/curated/en/794611627497650414/Transforming-Tourism-Toward-a-Sustainable-Resilient-and-Inclusive-Sector

World Bank. (June 2023). Tanzania Education and Skills for Productive Jobs Program (ESPJ). https://projects.worldbank.org/en/projects-operations/project-detail/P152810

World Bank. (2024). World Development Indicators. https://databank.worldbank.org/source/world-development-indicators

World Bank. (n.d.a). Dar es Salaam Maritime Gateway Project. https://projects.worldbank.org/en/projects-operations/project-detail/P150496

World Bank. (n.d.b). AFR RI-3A Tanzania-Zambia Transmission Interconnector. https://projects.worldbank.org/en/projects-operations/project-detail/P163752

YALI. (n.d.). What is YALI? Young African Leaders Association. https://www.yalieastafrica.org/

[1]Utafiti wa awali unalenga kutathmini miradi binafsi inayofadhiliwa na mashirika ya Serikali ya Marekani, na hahusishi masula ya mchango wa Marekani.

[2] Data ya fedha, imetumika ya kipindi cha kuanzia 2012 hadi 2022. Hii ni kwa sababu data inayohusiana na matokeo ya biashara, afya, elimu na uwekezaji, inahitaji muda mrefu ili matokeo yake yaweze kuonekana.

[3] PRC, UK, Japani, Kanada na Afrika Kusini

[4] Mashirika haya ni nguzo ya Maendeleo ya Afrika, Idara ya Kilimo, Idara ya Biashara, Idara ya Ulinzi, Idara ya Nishati, Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu, Idara ya Usalama wa Taifa, Idara ya Haki, Idara ya Kazi, Idara ya Nchi, Idara ya Jeshi, Idara ya Mambo ya Ndani, Idara ya Hazina, Idara ya Uchukuzi, Tume ya Biashara ya Shirikisho, Shirika la Changamoto za Milenia, Peace Corps, Shirika la Biashara na Maendeleo, na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani.

[5] Watoto na vijana wenye umri wa balehe wamefanywa yatima na na kuwekwa kwenye hatari ya kuambukizwa VVU na masuala mengine hatarishi.

[6] Mashirika haya yalijumuisha Shirika la Maendeleo ya Afrika, Idara ya Kilimo, Idara ya Ulinzi, Idara ya Nishati, Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu, Idara ya Usalama wa Nchi, Idara ya Haki, Idara ya Kazi, Idara ya Nchi, Idara ya Hazina, Peace Corps, Shirika la Biashara na Maendeleo, na USAID.

[7] Mashirika haya yalikuwa Hazina ya Maendeleo ya Afrika, Mfuko wa Mazingira Duniani, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa, Shirika la Kazi Duniani, UNAIDS, na UNICEF.

[8] Jina kamili la mradi ni Wezesha Ustawi, Endeleza Kiwango cha Elimu Kuzuia Ajira kwa Watoto/WEKEZA – Kusaidia Maisha na Kukuza Elimu Bora Ili Kukomesha Ajira kwa Watoto.

[9] Dhamana za uwekezaji au bima husaidia kudhamini makampuni dhidi ya hasara inayoweza kutokea kutokana na uwekezaji wao katika nchi nyingine ambako hawalijui soko (Gordon, 2008; Burgess na Custer, 2023).

[10] Dola za Kimarekani milioni 37.0 kwa mwaka 2022.

[11] Ili kushiriki katika mpango wa AGOA, takriban nchi 40 zilizolengwa zinatakiwa kutimiza masharti yanayohusiana na kuboresha utawala wao wa sheria, haki za binadamu, na kazi zenye viwango (Burgess na Custer, 2023). Hapo awali ilipitishwa kwa kipindi cha miaka minane, AGOA imefanywa upya mara mbili mwaka 2015 na tena mwaka 2018, na kudumu hadi 2025 (CRS, 2023).

[12] Chanzo kingine kinachojulikana ni Taasisi ya Elimu ya Kimataifa (IIE) ambayo inaonesha idadi ya chini kidogo. Hata hivyo, data yao inafafanua "mwanafunzi wa kimataifa kama mtu aliyeandikishwa katika kozi katika taasisi ya elimu ya juu iliyoidhinishwa, kw ajili ya kutunukiwa digrii nchini Marekani kwa viza ya muda inayoruhusu masomo ya kitaaluma." Hii itajumuisha watu binafsi kwenye viza ya F1. Licha ya takwimu hizo, data yetu inajumuisha watu binafsi wenye viza J1 (mabadilishano ya wageni) ambao wameidhinishwa kusoma, kuchunguza, kufanya utafiti na kupokea mafunzo, yasiyohusiha kutunukiwa shahada, nchini Marekani na/au wanafunzi. Tulipata data hii kutoka Idara ya Jimbo la Marekani na Idara ya Usalama wa Nchi ya Wanafunzi na Mfumo wa Taarifa ya mabadilishano ya Wageni wa Kubadilishana (SEVIS).

[13] Jumla hii inakokotolewa kwa kutumia data ya 2012 hadi 2022.

[14] Ili kukadiria michango ya hisani ya Marekani kwa Tanzania, tulitumia data kutoka kwenye kanzidata ya Mfumo wa Taarifa ya Mikopo ya OECD (CRS) kuhusu Wahisani binafsi wa Maendeleo (PPFD). Data hizi hujumuisha michango iliyoripotiwa kwa Tanzania kutoka taasisi za wahisani wa Marekani. Ingawa kuna uwezekano wa mashirika mengine muhimu ya hisani yenye makao yake makuu nchini Marekani, ripoti za michango kutoka kwa CRS zinatupa makadirio ya chini ya ukubwa wa michango ya hisani ya Marekani kwa Tanzania.

[15] Kwa kuzingatia wastani wa Dola za kimarekani kwa miaka kumi 2013-2022.

[16] OECD inafasili hisa za FDI kama thamani ya usawa wa wawekezaji wa kigeni katika na mikopo halisi ya biashara zilizopo kwenye taarifa za uchumi. Hisa za FDI ni kipimo cha jumla ya kiwango cha uwekezaji wa moja kwa moja kwa wakati husika.

[17] Masoko mengine 4 ya juu ni Kenya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Kuondoka kwa Wageni ya 2022 iliyochapishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania. Ripoti hiyo hiyo pia inatenganisha idadi ya wageni wa kimataifa wanaotembelea Zanzibar. Katika hali hii, masoko 5 ya juu ya chanzo cha watalii wa kimataifa yalikuwa Ufaransa, Ujerumani, U.K., Marekani na Uhispania.

[18] Kwa Tanzania Bara, wastani wa mgeni kutoka Marekani anatumia Dola 400 kwa usiku, ikilinganishwa na matumizi ya juu zaidi (watalii wa U.K. wanatumia wastani wa Dola 218 kwa kila mtu kwa usiku) (Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania, 2022). Kwa Zanzibar, wastani wa mtalii wa Kimarekani hutumia USD 495 kwa siku, ikilinganishwa na U.K. iliyoshika nafasi ya pili (USD 254/mtu/usiku).

[19] Kuanzia mwaka 2004, Tanzania ilianza kuzalisha gesi asilia ya kibiashara (Bishoge, et al., 2018). Uzalishaji wa ndani wa gesi asilia umeipa Tanzania fursa ya kuendeleza gesi asilia kama chanzo cha nishati kwa mitambo ya joto ambayo iliongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kuzalisha umeme. Kufikia mwaka wa 2011, gesi asilia ilipita nguvu ya maji kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na imepita nguvu ya maji tangu wakati huo.

[20] UNAIDS ilikadiria vifo vya VVU/UKIMWI vilivyoepukwa kutoka 2010 hadi 2022. Kabla ya 2010, makadirio ya vifo vya VVU/UKIMWI vilivyoepukika kwa kuondoa tofauti kati ya vifo vya mwaka 2006 (110,000) na makadirio ya vifo vya VVU/UKIMWI katika mwaka huo. Makadirio haya yanachukulia kuwa vifo vinavyotokana na VVU/UKIMWI kuanzia 2007 hadi 2009 vingebaki katika viwango vya 2006 kama kusingekuwa na utoaji wa ART.

[21] ART huzuia vifo vya moja kwa moja vya watu wenye UKIMWI na kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa kupunguza maambukizi ya VVU kwa wengine.

[22] Mnamo 2007, vifo 20,000 viliepukwa, na idadi hiyo iliongezeka hadi 68,000 mnamo 2022.

[23] WHO inafafanua kiwango cha "infant mortality" (vifo vya watoto wachanga chini ya mwezi mmoja) kama uwezekano wa mtoto kuzaliwa katika mwaka maalum au kipindi cha kufa kabla ya kufikia umri wa mwaka mmoja, ikiwa chini ya viwango vya vifo maalum vya umri wa kipindi hicho, kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa hai.

[24] WHO inafafanua kiwango cha "child mortality" (vifo vya watoto kuanzia mwaka mmoja) kama uwezekano kwamba mtoto aliyezaliwa katika mwaka au kipindi maalum atakufa kabla ya kufikia umri wa miaka 5, kulingana na viwango vya vifo maalum vya umri wa kipindi hicho, kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa hai.

[25] WHO inafafanua kiwango cha "neonatal mortality" (vifo vya watoto wachanga baada ya mwezi mmoja) kama idadi ya vifo wakati wa siku 28 za kwanza za maisha zilizokamilishwa katika mwaka fulani au kipindi kingine, kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa hai.

[26] Utafiti wa mtandaoni ulifanyika kwa kutumia Qualtrics. Kiwango cha sampuli ya Usikilizaji kwa Viongozi ya ndani ya AidData ilikuwa msingi wa sampuli ambayo iliongezewa anwani za ziada zinazofaa kwa kutumia vigezo vya taratibishi. Washiriki wa utafiti walichaguliwa kwa nyadhifa za uongozi ndani ya mashirika waliyofanyia kazi katika kipindi cha 2015-2024. Taarifa ya awali, mwaliko na makumbushio yalitumwa kwa watu 1,137, na watu 138 walijibu ili kushiriki kutoa maoni yao kupitia utafiti. Waliosailiwa katika utafiti huo ni pamoja na wawakilishi wenye ujuzi katika: kilimo na usalama wa chakula; demokrasia, haki za binadamu, na utawala; ukuaji wa uchumi na biashara; elimu; mazingira; usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake; afya; nishati; maji, usafi wa mazingira, na usafi; maendeleo ya kijamii; sayansi na teknolojia; viwanda na miundombinu; na nyinginezo. Asilimia sabini na tano ya wahojiwa walifanya kazi hasa katika bara la Tanzania; waliosalia ni pamoja na wale wanaofanya kazi Zanzibar au Zanzibar na Bara.

[27] Usaili ulifanyika kwa maafisa wakuu ambao walikuwa na uzoefu wa muda mrefu na ujuzi wa rasilimali za kifedha za taasisi zao. Kulikuwa na mwongozo wa usaili ambao ni wa wazi

[28] Wasailiwa waliulizwa swali lifuatalo: “Unakadiria kuwa mashirika ya serikali ya Marekani huchangia kiasi gani kwa Tanzania kila mwaka kwa wastani?” Waliojibu wanaweza kuchagua kutoka machaguo yafuatayo: chini ya dola milioni 100 (asilimia 9), dola milioni 100 hadi 500 (asilimia 30), dola milioni 500 hadi bilioni 1 (asilimia 31), na zaidi ya dola bilioni 1 (asilimia 30). Kama ilivyojadiliwa katika Sura ya 2, mashirika ya serikali ya Marekani hutoa milioni 673 kila mwaka kwa msaada wa moja kwa moja wa nchi mbili kwa Tanzania, ambayo ina maana kwamba wahojiwa wengi waliiona Marekani nzuri zaidi kuliko mchango wake halisi.

[29] Asilimia 61 ya waliohojiwa katika viashiria 6

[30] Asilimia 59 ya waliohojiwa katika viashiria 5